Connect with us

General News

Hatimaye Uhuru apunguza bei ya stima – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Hatimaye Uhuru apunguza bei ya stima – Taifa Leo

Hatimaye Uhuru apunguza bei ya stima

SERIKALI hatimaye imepunguza bei ya umeme siku moja baada ya Taifa Leo kukosoa Rais Uhuru Kenyatta kwa kutotimiza ahadi zake.

Wizara ya Kawi jana ilitangaza kupunguza bei ya umeme kwa asilimia 15.Serikali ilisema kuwa awamu ya pili ya punguzo hilo kwa asilimia 15 itatekelezwa kabla Machi, mwaka huu.

“Punguzo hilo la bei ya umeme litasaidia kuimarisha uchumi na kuboresha maisha ya Wakenya,” ikasema taarifa ya wizara ya Kawi.

Rais Kenyatta alikosolewa vikali kwa kushindwa kutekeleza ahadi ya kupunguza bei ya umeme ambayo amekuwa akitoa tangu 2018.

Rais Kenyatta alikosa kutekeleza ahadi aliyotoa Oktoba 20, ambapo aliahidi kuwa bei ya umeme ingepungua kwa asilimia 15 kufikia Disemba 24, mwaka jana.

Wakenya walikerwa na hatua ya Mamlaka ya Mafuta na Kawi (Epra) kujaribu kuongeza ushuri kwa umeme.

Katika hotuba yake ya kukaribisha Mwaka Mpya wa 2022, Rais Kenyatta alionekana kuashirikia kuwa bei ya umeme ingepunguzwa kuanzia Machi, mwaka huu.“Bei ya umeme itaendelea kupunguzwa zaidi kufikia robo ya kwanza ya mwaka wa 2022.”

Mnamo Oktoba 2018, Rais Uhuru Kenyatta alipokuwa akizungumza katika Chuo Kikuu cha Strathmore, aliagiza Waziri wa Kawi wakati huo, Bw Charles Keter, kupunguza bei ya umeme ndani ya mwezi mmoja.

“Lazima tushughulikie mambo ya stima, bei ya stima kwa ukweli kwa wenzetu wengi imepanda. Na leo hii mimi naamrisha waziri ndani ya mwezi mmoja apunguze bei ya stima ndio wananchi waweze kufanya biashara,” alisema Rais Kenyatta.