[ad_1]
Vincent Aboubakar afunga mabao mawili kuwapa wenyeji Cameroon ushindi wa 2-1 dhidi ya Burkina Faso
Na AFP
NAHODHA Vincent Aboubakar amefunga mabao mawili, yote yakiwa ni ya penalti, na kusaidia wenyeji Cameroon kuzamisha Burkina Faso 2-1 katika mechi ya ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Bara Afrika (AFCON 2021) jijini Yaounde, Jumapili.
Gustavo Sangare alikuwa ameiweka Burkina Faso kifua mbele uwanjani Olembe katika dakika ya 24 lakini mabao ya Aboubakar katika dakika ya 40 na lingine dakika tatu za majeraha baada ya 45 za kwanza, yaliwapa wenyeji sababu ya kutabasamu.
Rais waCameroon Paul Biya na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino wamekuwepo uwanjani kushuhudia gozi hilo.
Mashindano hayo yaliyoahirishwa mwaka 2021 kwa sababu ya janga la Covid-19 yataendelea hadi Februari 6, 2022.
[ad_2]
Source link