[ad_1]
VAR kutumiwa katika mechi zote 52 za AFCON nchini Cameroon
Na MASHIRIKA
TEKONOLOJIA ya VAR itatumiwa kwa mara ya kwanza katika mechi zote 52 za makala ya 33 ya fainali za Kombe la Afrika (AFCON) zinazoendelea nchini Cameroon.
Mnamo 2019 nchini Misri, VAR ilianza kutumiwa katika hatua ya robo-fainali za kipute hicho.
“Lengo letu ni kuimarisha viwango vya uamuzi katika kivumbi hicho ambacho pia kinatoa fursa kwa marefa wa haiba kudhihirisha ukubwa wa uwezo wao uwanjani. Hivyo, maamuzi ya kutumiwa kwa VAR katika mechi zote 52 ni mpango wa kimkakati katika juhudi za kufikia malengo ya kutoa waamuzi watakaokubalika kote ulimwenguni katika ulingo wa soka,” ikasema sehemu ya taarifa ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
CAF imeteua marefa 24, wasaidizi 31 na wataalamu wanane wa VAR kutoka mataifa 36 kwa ajili ya kipute cha AFCON mwaka huu. Salima Mukansanga kutoka Rwanda ni miongoni mwa marefa wanne wa kike katika orodha hiyo ya waamuzi.
Marefa wawili kutoka Shirikisho la Soka la Amerika ya Kati, Kaskazini na Caribbean (Concacaf), Mario Escobar kutoka Guatemala na mtaalamu wa VAR kutoka Mexico, Fernando Guerrero, pia amejumuishwa katika kundi la waamuzi watakaosimamia mechi za AFCON nchini Cameroon.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Next article
Mama awadunga wanawe kisu, mmoja afariki
[ad_2]
Source link