Connect with us

General News

Hofu ya ongezeko la matatizo ya kusikia nchini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Hofu ya ongezeko la matatizo ya kusikia nchini – Taifa Leo

SHINA LA UHAI: Hofu ya ongezeko la matatizo ya kusikia nchini

Na PAULINE ONGAJI

NI miezi miwili tangu Bi Fatuma*, mkazi wa mji wa Eldoret, ampeleke mwanawe wa umri wa miezi minne hospitalini ili kukaguliwa sikio lake, ambalo tangu utotoni limekuwa likimtatiza.

Mara ya mwisho alipoenda hospitalini, Bi Fatuma alishauriwa na daktari kwamba mwanawe anahitaji kifaa cha kumsaidia kusikia.

“Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa outocaustic emission, niliambiwa ataweza kusikia vyema kwa matumizi ya kifaa cha kumwezesha kusikia, na kuepuka matatizo zaidi ambayo huenda yakasababisha uziwi,” aeleza.

Lakini japo ni habari nzuri, Bi Fatuma bado ana wasiwasi kwani hana matumaini ya kupata pesa zinazohitajika kununua kifaa hicho.

“Tayari kwa matibabu na uchunguzi nimetumia zaidi ya Sh20,000, pesa ambazo nilipata kutoka kwa wahisani na marafiki. Kwa upande mwingine kifaa ninachoshauriwa ninunue kinagharimu zaidi ya Sh50,000 na zikiwa pesa ambazo sidhani nitazipata. Daktari ananiambia kwamba mwanangu yuko katika hatari ya kuwa kiziwi, lakini sina la kufanya,” aeleza.

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO, takriban watu milioni 466 duniani wanakumbwa na matatizo ya masikio ambayo yanasababisha uziwi, idadi hii inatarajiwa kuongezeka na kufikia asilimia 25 ifikapo mwaka wa 2050.

Takwimu zilizokusanywa kwenye aua ya kitaifa ya elimu maalum ya walemavu iliyotayarishwa mwaka wa 2014 na shirika la Voluntary Service Overseas (VSO Kenya), kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, zilionyesha kwamba viwango vya matatizo ya kusikia yanayosababisha uziwi, viliongezeka katika kipindi cha miongo miwili iliyopita. Aidha, zilionyesha kwamba 10% ya Wakenya wanakumbwa na tatizo hili.

Hii ni tofauti na mambo yalivyokuwa miongo miwili iliyopita, ambapo matatizo ya kusikia yalikadiriwa kuwakumba kati ya watu watano na wanane kati ya Wakenya 100.

WHO linaonya kwamba idadi ya Wakenya wanaokumbwa na tatizo la kuskia imeendelea kuongezeka ikilinganishwa na viwango vya kimataifa ambavyo ni watu watano kwa kila watu 100.

Wataalam wanahoji kwamba matatizo mengi yanayoathiri uwezo wa kusikia na hatimaye kusababisha uziwi hapa Kenya, yaweza kabiliwa endapo vifaa na huduma muhimu zitaimarishwa.

Kulingana na takwimu zilizokusanywa na Cristalfine ENT and Audiology Center, kliniki inayohusika na tiba ya sikio, pua na koo (ENT) mjini Eldoret, kwa wagonjwa 60 wanaozuru kituo hicho kila wiki, takriban nusu yao wanahitaji vifaa vya kuwawezesha kusikia.

Lakini miongoni mwa wagonjwa 30 wanaohitaji vifaa hivi, ni watano pekee wanaoweza kulipia kutoka mifukoni mwao.

“Kifaa kizuri cha kusaidia kusikia ni ghali mno ambapo bei yake huwa kati ya Sh55,000 na Sh100, 000, ambayo ni juu sana kwa mwananchi wa kawaida,” aeleza, Dkt Angela Wangare, mtaalam wa kupima na kutambua aina na kiwango cha kupoteza uwezo wa kusikia, katika Cristalfine ENT and Audiology Center.

Kulingana na Dkt Owen Menach, mtaalam wa ENT katika hospitali ya rufaa ya Moi, mjini Eldoret, kinachofanya mambo kuwa mabaya hata zaidi ni kwamba Bima ya Kitaifa ya Afya-NHIF haishughulikii gharama ya vifaa hivi, ambapo wagonjwa wengi wanalazimika kujinunulia.

Dkt Menach anasema kuna baadhi ya matatizo ya kusikia ambayo iwapo yatambuliwa na matibabu yanayofaa yasifuatwe, huenda yakasababisha uziwi.

“Wagonjwa wengi wamelazimika kukubali hatima ya kupoteza uwezo wa kusikia, na badala ya kutafuta usaidizi zaidi wa kimatibabu, wanaanza kujifunza lugha ya ishara,” aeleza Dkt Menach.

Dkt Wangare pia asema bei ya juu ya mashine zinazohitajika kufanya chunguzi tofauti za kutambua hatari ya kupoteza uwezo wa kusikia, imesababisha hospitali nyingi kukosa uwezo wa kutoa huduma zifaazo ili kukabiliana na matatizo ya kusikia.

 

Dkt Angela Wangare akichunguza ikiwa mgonjwa ana tatizo la kusikia akitumia mashine maalum – Brain Stem Evoked Response Audiometry Machine – katika kliniki ya Cristalfine Ear, Nose and Throat, and Audiology Centre mjini Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, Januari 10, 2022. PICHA | JARED NYATAYA

Kwa mfano, aeleza, katika eneo la Uasin Gishu, kliniki ya Cristalfine ENT, ndio kituo cha kipekee chenye uwezo wa kutoa huduma za uchunguzi kama vile pure tone audiometry ambao hutumika kupima kiwango cha kusikia au tympanometry, uchunguzi unaopima sehemu ya kati ya sikio na mwendo wa kiwambo cha sikio (ear drum).

Pia kliniki hii hutoa huduma za uchunguzi wa outocaustic emission (unaofanyiwa watoto wachanga na walio katika hatari ya kupoteza uwezo wa kusikia ili kutambua kiwango cha hatari ya kupoteza uwezo wa kusikia) .

“Pia, ni sisi ambao hufanya uchunguzi wa Brain Stem Evoked Response Audiometry (BERA); unaotumika kutambua pale ambapo tatizo la sikio linapotokea,” aongeza Bi Wangare.

Isitoshe, kituo hiki ndio pekee eneo hili chenye uwezo wa kutoa huduma za upatikanaji na usambazaji wa vifaa vya kuwezesha kusikia, huku wagonjwa kutoka kaunti zingine kama vile Bungoma, Nandi, Trans Nzoia, Busia, Kakamega na Vihiga, pia wakija hapa kupokea huduma. Ni suala ambalo mbali na kusababisha misongamano hospitalini, limefanya gharama ya huduma kuwa juu.

Kulingana na Dkt Menach, kwa yule mzazi ambaye hawezi mudu huduma za aina hii, hatima huwa kusubiri asijue la kufanya, na hivyo mtoto kupoteza uwezo wa kusikia kwa sababu ya tatizo ambalo laweza epukika.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending