Connect with us

General News

PSG na Lyon nguvu sawa katika Ligi Kuu ya Ufaransa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

PSG na Lyon nguvu sawa katika Ligi Kuu ya Ufaransa – Taifa Leo

PSG na Lyon nguvu sawa katika Ligi Kuu ya Ufaransa

Na MASHIRIKA

VIONGOZI wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), Paris Saint-Germain (PSG) walitoka nyuma na kulazimishia Olympique Lyon sare ya 1-1 ugenini mnamo Jumapili usiku.

Lyon waliwekwa kifua mbele na Lucas Paqueta katika dakika ya saba kabla ya Thilo Kehrer kutokea benchi na kusawazishia PSG katika dakika ya 76.

Kylian Mbappe wa PSG alishuhudia makombora yake mawili yakibusu mwamba wa lango la Lyon huku kiungo Marquinhos Correa akimshughulisha vilivyo kipa wa Lyon, Anthony Lopes.

Chini ya Mauricio Pochettino, PSG kwa sasa wanaongoza jedwali la Ligue 1 kwa alama 47 huku pengo la pointi 11 likitamalaki kati yao na Nice na Olympique Marseille wanaokamata nafasi za pili na tatu mtawalia. Lyon wanashikilia nafasi ya 11 kwa alama 25 sawa na Angers na Brest na sare dhidi ya PSG ilikuwa yao ya nne mfululizo.

Lionel Messi alikuwa miongoni mwa wanasoka wanne wa PSG waliokosa kunogesha mchuano huo baada ya kuambukizwa virusi vya corona.

Neymar Jr naye aliachwa nje kwa sababu bado anauguza jeraha la kifundo cha mguu ambalo linatarajiwa kumsaza mkekani kwa takriban wiki tatu zijazo. Bao la Kehrer lilikuwa lake la kwanza kambini mwa PSG tangu Februari 2020.

MATOKEO YA LIGUE 1 (Jumapili):

Lyon 1-1 PSG

Brest 0-3 Nice

Clermont 0-0 Reims

Metz 0-2 Strasbourg

Nantes 0-0 Monaco

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO