[ad_1]
Daktari ashtakiwa kwa kuuza barakoa feki
Na RICHARD MUNGUTI
DAKTARI na wafanyabiashara wawili pamoja na kampuni zao wameshtakiwa kwa kuiuzia Hospitali ya Aga Khan barakoa ghushi za thamani ya Sh11 milioni mwaka 2021.
Dkt Kimani Muthami, Bw William Muthee na Sylvia Wambui walifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi Bi Esther Kimilu na kukanusha mashtaka saba.
Watatu hao walishtakiwa pamoja na Lilian Awuor pamoja na kampuni yake ya Real Time Company.
Kampuni ya Dkt Muthami yanJohngray Communications Limited na Davetronics Company Limited yake Bw Muthee, zilishtakiwa.
Bi Awuor aliyeshtakiwa pamoja na Dkt Muthami na Bw Muthee hakufika kortini kwa madai sio buheri wa afya.
Washtakiwa hao walikana walikula njama ya kuuzia Hospitali ya Aga Khan vipande 20,000 vya barakoa zenye chapa ya “3M” bila idhini ya Kampuni ya 3M iliyoandikisha alama hiyo ya “3M”
Kesi hiyo imeorodheshwa kutajwa tena Februari 7, 2022 kwa maagizo zaidi.
Washtakiwa waliachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000.
Next article
AFC Leopards kusajili wanne mwezi huu
[ad_2]
Source link