Connect with us

General News

Mbinu za kudhibiti vifaabebe – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mbinu za kudhibiti vifaabebe – Taifa Leo

MALEZI KIDIJITALI: Mbinu za kudhibiti vifaabebe

MATUMIZI ya mitandao ya kijamii yanaongezeka na madhara yake kwa watoto yanaendelea kubainika.

Hata hivyo watalaamu wa malezi dijitali wanasema kwamba kuna mbinu zinazoweza kutumiwa na wazazi kudhibiti taarifa ambazo watoto wao wanatazama na muda wanaoweza kutumia mtandao.

“Kuna programu za kusaidia kudhibiti kizazi kipya cha digitali na waliounda wanasema zinasaidia wazazi kuwadhibiti watoto wao mtandaoni kwa urahisi zaidi,” asema mtaalamu wa masuala ya malezi dijitali, Sarah Kingston.

Anasema kuna mifumo kama mduara wa Disney, Koala Safe na Ikydz, ambayo inadaiwa kuwa na uwezo wa kudhibiti kila kifaa cha dijitali katika nyumba kupitia programu ya ‘smartphone’.

Anasema programu hizi zinaweza kuunganishwa kwa WiFi na kudhibitiwa mtu akiwa mbali na nyumbani kuhakikisha watoto wanalindwa na madhara ya kutazama habari na picha hatari kwenye mitandao ya kijamii. Mzazi pia anaweza kuchuja matumizi ya vifaa vya kidijitaji kulingana umri wa watoto.

“Kwa mfano, unaweza kuzuia watoto wako kutafuta wapenzi mtandaoni na kucheza kamari kwa kudhibiti vifaa vya kidijitali nyumbani hata ukiwa mbali kwa kuwa kuna programu zinazokuwezesha kuona wanachofanya na kila kifaa kupitia simu yako,” aeleza Kingston.

Unaweza pia kusitisha intaneti kwa muda fulani na kupanga muda wa kulala wa watoto wako kama mbinu ya kuhakikisha hawatekwi na mtandao.

Wataalamu wanasema intaneti inaweza kuwa chanzo kizuri, lakini pia inaweza kuwa kama msitu wa wanyama kwa watoto na si sawa kuwaacha mbugani bila ulinzi.

“Kwa namna hiyo, mzazi hafai kufikiria kuwa ni sawa kwa watoto kuzurura kwenye intaneti bila mwongozo au masharti yoyote,” asema Kingston.

Hata hivyo, wanasema kuwa baadhi ya programu za kudhibiti intaneti hazifanyi kazi watoto wakiondoka nyumbani mbali na WiFi na havitafanya kazi iwapo WiFi imezimwa au kama hauna data katika simu kukuwezesha kupata huduma za intaneti.