Connect with us

General News

Bodi ya KPLC yapigwa darubini kuhusu kupotea kwa umeme – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Bodi ya KPLC yapigwa darubini kuhusu kupotea kwa umeme – Taifa Leo

Bodi ya KPLC yapigwa darubini kuhusu kupotea kwa umeme

Na VINCENT ACHUKA

WAPELELEZI sasa wanawaelekezea lawama wakurugenzi wa bodi ya kampuni ya umeme nchini (KPLC) baada ya kubainika kuwa mojawapo ya sababu zilizochangia kupotea kwa umeme nchini majuzi ni hasira miongoni mwa wafanyakazi kuhusu mpango wa kuwafuta kazi.

Aidha, ilisemekana hitilafu hiyo ilisababishwa na utepetevu na kukatwa kwa vyuma katika nguzo za kupitishia umeme na wahalifu wenye nia ya kuviuza kwa waendeshaji biashara ya vyuma vikuukuu.Polisi wanachukulia tukio hilo la kupotea kwa umeme kama tishio kwa usalama na uthabiti wa kitaifa.

Jumatano, Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) ilisema huenda wafanyakazi 10 wa KPLC waliofikishwa mahakamani kuhusiana na tukio hilo, wakashtakiwa si tu kwa kosa la hujuma bali ugaidi.

“Hujuma hiyo iliyoonekana kupangwa ilisababisha usumbufu, uharibifu wa biashara na kuvurugwa kwa hudumu muhimu ambayo ingesababisha vifo,” DCI ikasema.

Kulingana na Sheria ya Kupambana na Ugaidi, kitendo cha kigaidi ni “kitendo kinachovuruga mfumo wa upitishaji umeme na kuchangia kukatizwa ka mawasiliano na huduma za kifedha, uchukuzi na huduma zingine muhimu.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa baadhi ya wafanyakazi na wanachama wa bodi ya KPLC wameingiwa na wasiwasi tangu serikali ilipoanzisha mabadiliko katika Wizara ya Kawi, hususan kampuni hiyo.

Vile vile, kuna shauku kuwa huenda baadhi ya kampuni za kibinafsi za kuzalisha umeme (IPP), ambazo faida zao zimepungua kufuatia hatua ya serikali kupunguza bei ya stima, zilishirikiana na baada ya wafanyakazi wa KPLC kuihujumu.

Ijumaa Waziri wa Kawi Monica Juma alisisitiza kuwa kandarasi zote zitajadiliwa upya kwa lengo la kupunguza bei ya stima kutoka IPPs. “Kuna sehemu ya kandarasi inayosema kuwa inaweza kubadilishwa baada ya muda fulani,” akasema Dkt Juma.

Mabadiliko katika sekta ya kawi yaliyoanza Oktoba mwaka jana Dkt Juma alipochukua usimamizi wa Wizara ya Kawi, hayajawafurahisha baadhi ya maafisa wa KPLC.

Mnamo Ijumaa, Waziri aliendelea kusisitiza kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo waliopotoka kimaadili na ambao ni wazembe hawatasazwa. Mnamo Oktoba Waziri huyo aliamuru kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi kadha wa KPLC.

Miongoni mwao walikuwa; Imelda Bore, Charles Cheruiyot, Peter Wambua, Aggrey Machasio, Cecilia Kalungu, Peter Njenga, Robert Mugo, Thomas Ogutu, Stephen Vikiru, John Ngeno, Charles Mwaura na Jeremia Kiplagat.