Connect with us

General News

MCK yataka wanasiasa wanaovamia wanahabari wazimwe kuwania viti 2022 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

MCK yataka wanasiasa wanaovamia wanahabari wazimwe kuwania viti 2022 – Taifa Leo

MCK yataka wanasiasa wanaovamia wanahabari wazimwe kuwania viti 2022

NA SAMMY WAWERU

BARAZA la Vyombo vya Habari Nchini (MCK) linapendekeza wanasiasa wanaovamia wanahabari katika mikutano ya kisiasa na umma kupigwa marufuku kushiriki uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

MCK imesema haitaendelea kufumba macho wanahabari kuhujumiwa na viongozi na wanasiasa.

Chama hicho kimetangaza kwamba kitaiandikia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kuadhibu wanasiasa watakaopatikana na hatia.

“Tutaandikia IEBC barua viongozi na wanasiasa wanaopiga waandishi wa habari kuzuiwa kugombea viti wanavyomezea mate,” akasema Bw Victor Bwire, Mkurugenzi mafunzo ya wanahabari MCK.

Visa vya waandishi kupokea vitisho kutoka kwa wanasiasa na hata kupigwa na wafuasi wao katika mikutano ya hadhara, vimeanza kuripotiwa.

“Hatutanyamaza wanabahari wakikandamizwa na kuhujumiwa,” Bwire akasisitiza.

Afisa huyo alisema hayo Jumapili jioni, katika mahojiano na runinga ya KTN News.

Walinzi wa viongozi na wanasiasa pia wanalaumiwa kudhulumu wanahabari wakitekeleza majukumu yao kukusanya habari, hasa katika mikutano ya umma.

Huku taifa likijiandaa kushiriki uchaguzi mkuu 2022, Bw Bwire alisema MCK itaendelea kutoa mafunzo kwa vyombo vya habari na waandishi wake kuripoti kwa njia inayofaa kampeni, kabla na wakati wa uchaguzi.

Katika kipindi hiki ambapo mitandao ya kijamii imekumbatiwa kwa kiwango kikubwa, waandishi wa habari wanahimizwa kuwa makini na baadhi ya habari potovu zinazoezwa kwenye majukwaa.

Pamoja na wahariri, wanashauriwa kupiga msasa habari na jumbe kabla kuzichapisha magazetini, kwenye tovuti, kupeperusha katika runinga na redio.

Baadhi ya mabloga na watumizi wa mitandao, wanatumia umaarufu wao mitandaoni kuharibia jina viongozi na wanasiasa wanaotofautiana nao kimtazamo na kimawazo.

Vyombo vya habari vihimize meza za wahariri kuchunguza kwa kina uhalisia wa habari wanazopokea, hususan za kisiasa.