Connect with us

General News

UAE yaondoa marufuku ya safari za ndege za abiria kutoka Kenya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

UAE yaondoa marufuku ya safari za ndege za abiria kutoka Kenya – Taifa Leo

UAE yaondoa marufuku ya safari za ndege za abiria kutoka Kenya

Na WANGU KANURI

WASAFIRI kutoka Kenya watakubaliwa kuingia Dubai kutoka Jumamosi, Januari 29, 2022.

Hii ni baada ya dola la Milki za Kiarabu (UAE) kuondoa marufuku lililoweka mwaka 2021 ya kuzuia ndege kutoka baadhi ya nchi za Afrika.

Vile vile, wasafiri kutoka nchi za Tanzania, Ethiopia, Nigeria, Kongo, Afrika Kusini, Botswana, Lesotho, Msumbiji, Namibia na Zimbabwe pia wataruhusiwa kuingia UAE ilhali wale kutoka nchi za Uganda, Ghana na Rwanda watahitajika kuafikiana na masharti ya Dubai ya kuingia nchini humo.

Wasafiri hao watahitajika kuonyesha cheti kinachoonyesha kuwa hawana virusi vya Covid-19 na msimbo wa QR uliofanywa katika kituo cha afya kinachoaminika chini ya saa 48 au kwenye kituo cha ndege saa sita kabla hawajaondoka nchini mwao.

Zaidi ya hayo, wasafiri hao watahitajika kupimwa ili kutathmini kama wana virusi vya Covid-19 pindi tu wafikapo Dubai.

Jumanne, Kenya iliondoa marufuku iliyokuwa imeweka wiki mbili zilizopita, ikiwakataza wasafiri kutoka UAE kufika nchini.

Mapema mwaka huu 2022, Kenya iliweka marufuku hayo kama njia ya kulipiza baada ya Dubai kuweka marufuku ya ndege kutoka Kenya huku ikidai kuwa vyeti vilivyowasilishwa na Wakenya vilikuwa feki.

Hata ingawa marufuku hayo hayakuathiri ndege za mizigo, kuondolewa kwake kuliwafaa sana mamia ya wasafiri katika nchi hizo mbili.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending