Connect with us

General News

Wauzaji pombe Kiambu wapunguziwa ada ya leseni kwa asilimia 20 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wauzaji pombe Kiambu wapunguziwa ada ya leseni kwa asilimia 20 – Taifa Leo

Wauzaji pombe Kiambu wapunguziwa ada ya leseni kwa asilimia 20

Na LAWRENCE ONGARO

WAMILIKI wa baa na sehemu nyingine za burudani katika Kaunti ya Kiambu, wamepata afueni baada ya serikali ya kaunti kupunguza kwa asilimia 20 kiwango cha fedha za kulipia leseni.

Ujumbe huo ulitolewa na Gavana wa Kiambu Dkt James Nyoro, alipofanya kikao mjini Kiambu na wamiliki wa biashara hizo.

Wanachama wa chama cha wauzaji pombe na mvinyo na wenye mikahawa kutoka kaunti ndogo 12 za Kiambu walipongeza juhudi za gavana huyo kupunguza ada.

Dkt Nyoro alieleza kuwa alichukua hatua hiyo kutokana na jinsi Covd-19 ilivyoathiri biashara nyingi katika kaunti hiyo.

“Tunaelewa biashara nyingi ziliathirika na kwa hivyo ni vyema kujali wafanyabiashara hao waweze kujimudu,” alieleza Dkt Nyoro.

Alizidi kueleza kuwa serikali yake itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wote hasa wanaouza pombe.

Alisema hata ingawa mambo bado ni magumu, ni vyema kuzingatia sheria za afya ili kupunguza makali ya Covid-19.

“Wakenya watalazimika kukabiliana na Covid-19, huku pia wakiendesha biashara zao kwa sababu homa hiyo tutaendelea kuishi nayo kwa muda,” alifafanua gavana huyo.

Biashara zinazoendeshwa katika miji mikubwa zitalipa ada ya Sh48,000 badala ya Sh60,000.

Zile zinazoendeshwa katika miji midogo zitalazimika kulipa ada ya Sh32,000 badala ya Sh40,000.

Halafu katika maeneo ya mashinani, watalazimika kulipa Sh19,200 badala ya Sh24,000.

Na katika maeneo ya burudani na hoteli zinazostahili kulipa Sh100,000 sasa wamepunguziwa hadi Sh80,000. Katika miji midogo, biashara zilizolipa Sh80,000 zitatakiwa kulipa Sh64,000. Halafu mashinani watalipa 48,000 badala ya 60,000.

Nazo hoteli kubwa zinazoendesha biashara ya baa, zitalipa Sh121,600 badala ya Sh152,000.

Halafu vilabu vikubwa vitalazimika kukohoa Sh128,000.

Supamaketi ambazo zinauza mvinyo na pombe zitalazimika kulipa Sh156,000.

Mkurugenzi anayehusika na utoaji leseni hizo Bw Michael Kang’ethe, aliwahimiza washika dau wote wanaoendesha biashara hizo kufuata sheria zote zilizowekwa na kulipa fedha hizo bila kuchelewa.

Alitoa onyo kwa maafisa wa ukaguzi wa bidhaa hizo, wanaohangaisha wafanyabiashara hao kuwa watakabiliwa vilivyo.

Naye mwenyekiti wa chama cha wauzaji pombe Bw William Muiko, alipongeza gavana Nyoro kwa kupunguza kiwango cha ada hiyo aliyotaja kama mwelekeo mzuri kwa wafanyabiashara.