Connect with us

General News

Shujaa yahafamu wapinzani wake wa Kombe la Afrika – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Shujaa yahafamu wapinzani wake wa Kombe la Afrika – Taifa Leo

Shujaa yahafamu wapinzani wake wa Kombe la Afrika

Na GEOFFREY ANENE

KENYA imetiwa katika orodha ya mataifa 14 yatakayowania tiketi moja ya kushiriki Kombe la Dunia la raga ya wachezaji saba kila upande ya wanaume kutoka mchujo wa Afrika mnamo Aprili 23-34 jijini Kampala, Uganda.

Mabingwa watetezi Kenya wameshiriki makala yote tano yaliyopita ya Kombe la Dunia nchini Argentina (2001), Hong Kong (2005), Milki za Kiarabu (2009), Urusi (2013) na Amerika (2018).

Vijana wa kocha Innocent Simiyu walijipata katika mchujo wa Afrika baada ya kukamilisha Kombe la Dunia 2018 nje ya timu nane-bora zilizofuzu moja kwa moja.

Kenya maarufu kama Shujaa, sasa itashiriki kombe la Afrika kutafuta tiketi dhidi ya Burkina Faso, Ghana, Madagascar, Namibia, Senegal, Tunisia, Uganda na Zimbabwe pamoja na mshindi na nambari mbili wa zoni ya Kusini na pia kati.

Mashindano ya kuingia Kombe la Afrika ya zoni ya Kusini yameratibiwa kufanyika nchini Lesotho mnamo Januari 29-30. Yanakutanisha Mauritius, Botswana, Eswatini na Lesotho.

Kwa sasa, Shujaa iko nchini Uhispania kwa Raga za Dunia duru ya Seville Sevens. Iliaibishwa 42-0 katika mechi yake ya ufunguzi ya Kundi D dhidi ya Australia. Imechapa Canada 24-5 katika mechi ya pili. Itamenyana na Scotland saa kumi jioni Jumamosi kuamua nani kati ya wawili hao ataungana na Australia katika robo-fainali kuu.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending