Connect with us

General News

Burkina Faso wang’oa Tunisia kwenye robo-fainali – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Burkina Faso wang’oa Tunisia kwenye robo-fainali – Taifa Leo

AFCON: Burkina Faso wang’oa Tunisia kwenye robo-fainali

Na CHRIS ADUNGO

TINEJA Dango Ouattara alifunga bao la pekee lililowapa Burkina Faso ushindi wa 1-0 dhidi ya Tunisia kabla ya kufurushwa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika ya 82.

Ouattara, 19, alipokezwa krosi na Blati Toure kabla ya kuacha hoi mabeki wawili wa Tunisia waliokuwa wakiwania taji la pili la Kombe la Afrika (AFCON) mwaka huu tangu watawazwe wafalme mnamo 2004 wakiwa wenyeji.

Alionyeshwa kadi nyekundu dakika nane kabla ya kipenga cha mwisho kupulizwa baada ya kumpiga kumbo Ali Maaloul.

Burkina Faso almaarufu ‘The Stallions’ hawajawahi kushinda taji la AFCON. Sasa watakutana na mshindi kati ya Senegal na Equatorial Guinea watakaomenyana katika robo-fainali nyingine mnamo Januari 30, 2021.

Hata hivyo, watakosa huduma za Ouattara ambaye sasa anatumikia marafuku. Tunisia walilalamikia kunyimwa penalti mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya Soumaila Ouattara kumkabili visivyo Wahbi Khazri ndani ya kijisanduku.

Burkina Faso ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya 60 kimataifa, wameshinda mechi zote za robo-fainali za AFCON ambazo wamewahi kushiriki, zikiwemo tatu kutokana na makala manne yaliyopita. Tunisia wanaoorodheshwa wa 30 duniani, wamepoteza robo-fainali sita kati ya saba zilizopita kwenye kipute hicho.

The Carthage Eagles wa Nigeria walifuzu kwa hatua ya robo-fainali baada ya kudengua Nigeria kwa kichapo cha 1-0 katika raundi ya 16-bora mnamo Januari 23, 2022.

Burkina Faso walipokezwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Nigeria kwenye fainali ya AFCON 2013 nchini Afrika Kusini. Nusura wafunge bao la pili mwishoni mwa kipindi cha pili ila Cyrille Bayala akazidiwa maarifa na kipa Bechir Ben Said wa Tunisia.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO