Connect with us

General News

Mwanaharakati aliyezima BBI sasa kugombea useneta Migori – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwanaharakati aliyezima BBI sasa kugombea useneta Migori – Taifa Leo

Mwanaharakati aliyezima BBI sasa kugombea useneta Migori

Na IAN BYRON

MWANAHARAKATI wa Migori aliyekata rufaa ya kusimamisha Mpango wa Maridhiano (BBI) katika Mahakama ya Rufaa, amejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania useneta wa Kaunti ya Migori.

Bw Isaac Aluochier hata hivyo anasema hatashiriki mchujo wa kuwania tiketi ya chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga kwa sababu ya “ubaguzi”.

Bw Aluochier amefichua kwamba alikuwa amepanga kugombea ugavana lakini akabadilisha nia na kuamua kugombea useneta anaosema hauna ushindani mkali wala gharama kubwa.

“Nilitaka kugombea kiti cha ugavana lakini kampeni za kiti hicho ni ghali. Kwa kuwa sina pesa nyingi za kupiga kampeni, nimeamua kugombea useneta,” Aluochier alisema.

Aliongeza: “Kiti hicho hakijavutia washindani wakali na nina hakika nitashinda. Hili ndilo jukwaa zuri la kuwakilisha watu wa Migori kwa kuwa nina rekodi ya kuwa mtetezi wa haki za binadamu.”

Alisema kutokana na rekodi yake, ndiye anastahili kumrithi Seneta wa sasa Ochillo Ayacko anayegombea ugavana wa Migori.

Alisema aliamua kutojiunga na ODM akidai chama hicho hakina demokrasia.

Atatumia tiketi ya chama cha Justice and Freedom Party kugombea kiti hicho.