Connect with us

General News

Madaktari waahirisha mgomo baada ya kaunti kuahidi kuwalipa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Madaktari waahirisha mgomo baada ya kaunti kuahidi kuwalipa – Taifa Leo

Madaktari waahirisha mgomo baada ya kaunti kuahidi kuwalipa

NA LUCY MKANYIKA

WAHUDUMU wa afya katika Kaunti ya Taita Taveta, wameamua kuahirisha mgomo wao baada ya serikali ya kaunti hiyo kuwaahidi kuwalipa mishahara yao iliyochelewa.

Maafisa wa vyama vinavyowakilisha wahudumu wa afya walikutana na wale wa serikali ya kaunti Jumatatu jioni, wakaelewana kuwa mishahara wanayodai italipwa kabla wiki hii ikamilike.

“Tulikutana tukakubaliana mishahara italipwa wiki hii tukiendelea kutatua suala kuhusu bima zao,” akasema Waziri wa Afya katika kaunti, Bw John Mwakima.

Viongozi wa Chama cha Wahudumu wa Matibabu, Wafamasia na Madaktari wa Meno (KMPDU), kile cha wauguzi (KNUN) na cha maafisa wa utabibu (KUCO) walikuwa wameambia wanachama wao waanze mgomo baridi hadi wakati serikali ya kaunti itakapotatua lalama zao.

Vyama vingine vilivyokuwa vimepanga kushiriki mgomo huo ni kile cha maafisa wa maabara za matibabu (KNUMLO) na wanateknolojia za ufamasia (KNUPT).

Mratibu wa KMPDU katika tawi hilo, Dkt Richard Wangai, alisema watasubiri kuona ikiwa malalamishi yao yatasuluhishwa.

“Tutakutana nao tena Jumatatu ijayo. Walisema tuwape wiki moja ili watatue masuala ya mishahara na bima ya matibabu. Tunatumai tutapata suluhisho mwafaka, la sivyo tutaanza mgomo wetu,” akasema.

Walikuwa wamelalamika pia kwamba pesa wanazokatwa hazitumwi kwa taasisi zinazostahili, huku pia kukiwa na uhaba wa dawa na mahitaji mengine ya kutoa huduma hospitalini.

Hata hivyo, Bw Mwakima alisema tatizo lilisababishwa na jinsi serikali ya kitaifa ilichelewa kutuma pesa kwa kaunti, hali ambayo alisema imeathiri utoaji huduma hospitalini.

Alithibitisha kuwa bima ya afya ya wahudumu wa afya ilipitwa na wakati Januari 24 na haingeongezewa muda kwa sababu ya ukosefu wa fedha.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending