Connect with us

General News

Kaunti yaambia wakazi wazoee usafiri wa ‘2/2/22’ – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kaunti yaambia wakazi wazoee usafiri wa ‘2/2/22’ – Taifa Leo

Kaunti yaambia wakazi wazoee usafiri wa ‘2/2/22’

WINNIE ATIENO na FARHIYA HUSSEIN

SERIKALI ya Kaunti ya Mombasa imesema misongamano iliyoshuhudiwa barabarani Jumatano itapungua kwani inatarajiwa wakazi watazoea mtindo mpya wa 2/2/22.

“Tulitabiri kungekuwa na matatizo siku ya kwanza lakini watu watazoea kadri muda unavyosonga. Kutakuwa pia na changamoto ya steji lakini tutatenga sehemu zao baadaye,” Waziri wa Barabara, Miundomsingi na Ujenzi katika Kaunti, Bw Tawfiq Balala, akasema.

Alisema hayo huku baadhi ya wadau wakitaka mfumo huo uliosababisha baadhi ya barabara muhimu kugeuzwa kuwa za kuelekea upande mmoja pekee, uwaziwe upya.

Barabara zilizoathirika zaidi kwa misongamano Jumatano ni ile ya kuingilia na kutoka kisiwani, kwa mfano inayounganishwa na Daraja la Nyali.

Licha ya maafisa wa trafiki wa Kaunti na polisi kuongezwa barabarani, baadhi ya madereva walichanganyikiwa katikati ya mji kuhusu barabara walizofaa kutumia na hivyo kufanya magari kusafiri polepole.

Wahudumu wa matatu za maeneo tofauti walilazimika kupandisha nauli kwani iliwachukua muda mrefu kuliko kawaida kukamilisha safari moja.

Mamlaka ya Barabara za Kitaifa nchini (KeNHA) ilikosoa mtindo huo mpya.

“Barabara zinazosimamiwa na KeNHA zimeathiriwa na pendekezo hilo jipya. Hizo ni barabara muhimu zinazohudumia magari mengi,” akasema meneja wa KeNHA, eneo la Pwani, Bw Eric Wambua.

Hata hivyo, Bw Balala, alisema usimamizi wa trafiki ni jukumu la serikali za kaunti.

Mkuu wa polisi wa trafiki eneo la Pwani, Bw Peter Maina, alisema baada ya siku tatu utathmini utafanywa kubainisha kama kuna chochote kitakachohitaji kubadilishwa.

Mratibu wa Chama cha Wamiliki wa Matatu, Bw Salim Mbarak, na Mkurugenzi wa Chama cha Wachukuzi Kenya, Bw Ahmed Juneja, walikosoa mpango huo na kusema haukushirikisha umma kamwe.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending