Connect with us

General News

Uzinduzi wa programu ya kutega uchumi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Uzinduzi wa programu ya kutega uchumi – Taifa Leo

Uzinduzi wa programu ya kutega uchumi

Na WANGU KANURI

KAMPUNI ya Waanzilishi ilizindua programu ya Ndovu inayoratibiwa na Mamlaka ya Kusimamia Biashara ya Hisa (CMA) Jumatatu kwa lengo la kuwasaidia Wakenya kuwekeza akiba zao kupitia hisa za kampuni, dhamana ya akiba na soko la hisa la ETF.

Akiwahamasisha walioungana katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa programu ya Ndovu, Bi Radhika Bhachu, alisema kuwa programu hiyo itarahisisha uwezo wa kununua au kuuza kwenye soko za fedha za kimataifa kwa siku tatu.

“Programu hii ipo kwenye tovuti ya Ndovu na Play Store na humruhusu mtu kuwekeza Sh5,000 au zaidi,” akasema.

Vile vile Bi Bhachu alieleza kuwa uwekezaji wa pesa leo, huwa akiba ya kesho kulingana na riba inayotozwa kupitia nyanja tofauti za kutega uchumi.

Hata hivyo, programu hiyo huwawezesha watu kutoa pesa zao kwa wakati wowote ule, ila tu siku tatu baada ya kupatiana notisi.

“Programu ya Ndovu imewafaa wananchi walio kwenye Afrika Mashariki na baada ya mwaka mmoja, iwapo utakuwa umewekeza pesa zako kwenye soko za Amerika, pesa zako zitakuwa zimepata riba kwa asilimia 12,” akasema Afisa Mkuu wa Biashara, Ro Nyangeri.

Ukosefu wa ufahamu kuhusu uwekezaji akiba umewafanya Wakenya wengi kutopangia siku zao za usoni.

Vile vile, Wakenya kuhadaiwa na kampuni za utegaji uchumi kumewafanya wengi kuweka akiba zao kwenye benki.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending