[ad_1]
TAHARIRI: Serikali inafanya mzaha na mtaala wa CBC
NA MHARIRI
INASIKITISHA kuwa huku inaposalia miezi 11 pekee kabla ya mkumbo wa kwanza wa wanafunzi wanaosoma chini ya Mtaala mpya wa Umilisi (CBC), serikali inaonekana kutojiandaa kikamilifu.
Ni mzaha unaojidhihirisha wazi kuwa bado serikali haijatenga pesa za kufadhili masomo ya wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Kwanza (Gredi ya 7) kuanzia Januari 2023.
Vilevile, serikali haijatoa mwongozo kikamilifu kuhusu ni wapi wanafunzi hao wataendelezea masomo yao katika kidato hicho cha kwanza.
Kwa kauli hii ya pili ninamaanisha, haijabainika wazi iwapo wanafunzi hao, hasa wale wanaosomea katika shule za kibinafsi, watayaendeleza masomo yao katika shule zizo hizo za msingi wanazosomea au watajiunga na shule za upili zilizoko sasa, za mfumo wa 8-4-4, ambazo katika utaratibu wa mtaala mpya wanafaa wajiunge nazo wakiwa katika gredi ya 9.
Naam, Serikali imetangaza kutoa takribani Sh10 bilioni za ujenzi wa madarasa mapya kwa ajili ya wanafunzi hao wa Gredi ya 7.
Lakini haijatoa mwongozo bainifu kuhusu shule za kibinafsi.
Mbali na hilo, suala linaloshangaza hata zaidi ni kwamba serikali haijatenga pesa za elimu ya bure kwa wanafunzi hao wa Gredi ya 7 katika bajeti yake.
Kila mwanafunzi anahitaji karibu Sh28,000.
[ad_2]
Source link