Connect with us

General News

Jubilee na ODM kufanya mchujo pamoja – Junet – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jubilee na ODM kufanya mchujo pamoja – Junet – Taifa Leo

Jubilee na ODM kufanya mchujo pamoja – Junet

VYAMA vya Jubilee na ODM vinafanya mazungumzo kwa lengo la kufanya mchujo wa pamoja chini ya mwavuli wa Azimio la Umoja, kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Wakiongea katika maeneo tofauti katika kaunti ya Migori, mkurugenzi wa uchaguzi wa ODM Junet Mohamed na Katibu Mkuu wa Jubilee Raphael Tuju walifichua kuhusu mipango hi – yo wakisema itapiga jeki ndoto ya urais ya kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Bw Junet, ambaye alion – gea na wanahabari katika eneobunge lake la Suna Mashariki jana, alisema vyama hivyo vitafanya mchujo wa pamoja baada ya mkataba wa kuunda muungano wa Azimio la Umoja kutiwa saini.

“Tutafanya mchujo wa pamoja chini ya muungano wa Azimio la Umoja kwa sababu sisi ni

washirika. Aidha, tutaendesha shughuli za kisiasa na kuendesha serikali pamoja,” akasema.

Bw Junet alisema hatua hiyo itaidhinishwa chini ya muungano na ushirika kati ya vyama hivyo viwili ambao utaendelezwa kwa kipindi kirefu.

Mbunge huyo alielezea Imani yake kuwa ODM na Jubilee wataunda serikali ijayo baada ya mgombeaji wao wa urais Raila Odinga kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu ujao.

Bw Junet ametoa kauli hiyo wiki moja baada ya Bw Tuju kudokeza kuwa chini ya muungano wa Azimio la Umoja, vyama hivyo vitadhamini wagombeaji, pamoja, katika nyadhifa nyingine mbali na urais.

Bw Tuju ambaye aliungana na viongozi wengine kuendesha hamasisho kuhusu usajili wa wapigakura wapya alisema vyama hivyo vitadhamini wagombeaji pamoja ili kuzuia ushindani kati yavyo.

“Tunajadili mikakati ambayo itatuwezesha kufanya kazi chini ya muungano. Kwa kuwa tuko katika Azimio la Umoja, tunawazia kutodhamini wagombeaji katika ngome za ODM. Suala hili, hata hivyo, litajadiliwa zaidi baadaye,” Bw Tuju akasema Jumamosi.

Katibu huyo mkuu wa Jubilee pia alisema chama hicho tawala kitatarajia ODM kutodhamini wagombeaji katika ngome zao, haswa maeneo ya Mlima Kenya.

“Kwa kufanya hivyo, tutahakikisha kuwa Bw Odinga ameshinda urais tena kwa idadi kubwa ya wajumbe katika Bunge la Kitaifa, Seneti na mabunge ya kaunti,” Bw Tuju akaeleza.

Tuju alitumia nafasi hiyo kuwahimiza viongozi wa Luo Nyanza kuendelea kuwahimiza wakazi kujiandikisha kuwa wapigakura hata baada ya muda uliotengwa kukamilika.

“Hata baada ya kipindi kilichotengwa na IEBC kukamilika, nawaomba muwahimize wananchi ambao wataachwa nje baada ya awamu ya pili kukamilika Februari 5, 2022, kwamba bado wanaweza kujiandikisha katika afisi za IEBC ka – tika maeneobunge,” akaeleza.

“Huu ndio wakati wa viongozi waliochaguliwa na wale wanaowania viti katika eneo la Luo Nyanza kuhakikisha kuwa watu wengi wanajiandikisha kuwa wapiga kura ili Bw Odinga aweze kushinda,” Bw Tuju akasema.

Katibu huyo mkuu wa Jubilee aliwasuta wanasiasa ambao wanatumia picha na jina la Bw Odinga kusaka uungwaji mkono kutoka kwa wananch huku wakichelea kuendesha kampeni za kuwahimiza raia wajiandishe.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending