Connect with us

General News

Kiboko bado ni hatia shuleni, Magoha aonya walimu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kiboko bado ni hatia shuleni, Magoha aonya walimu – Taifa Leo

Kiboko bado ni hatia shuleni, Magoha aonya walimu

NA WINNIE ATIENO

WAZIRI wa Elimu, Prof George Magoha, sasa amewaonya walimu na wakuu wa shule dhidi ya kuchapa wanafunzi akisisitiza kuwa ni hatia.

Prof Magoha, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipigia debe kurudishwa kwa adhabu ya viboko shuleni, aliwasihi maafisa wa polisi kuwakamata walimu na wakuu wa shule wanaowatandika wanafunzi hadi kuwajeruhi.

Hata hivyo, alisema walimu wanaweza tu kuchapa mwanafunzi iwapo anamtishia maisha ya mwalimu.

“Kuna wanafunzi wengine ambao huwa wanatishia walimu. Kama

ni hali aina hiyo inaeleweka lakini usijaribu kumchapa mwanafunzi, utakamatwa upelekwe jela,” alisema alipoenda kukagua shule ya upili ya Allidina Visram mjini Mombasa, Jumapili.