Wafuasi wa Ruto wadai wanazuiwa kuhama Jubilee
NA VITALIS KIMUTAI
WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamedai kwamba wanachama wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) wamezuiwa kuhama chama cha Jubilee kabla ya mchujo wa vyama vya kisiasa.
Wanataka Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) kuhakikisha kujiuzulu, kuhama na kujisajili kama mwanachama wa chama cha kisiasa kunafanyika bila tatizo ili kuepuka mizozo na taharuki za kisiasa.
Bw Ronald Tonui, mbunge wa Bomet ya Kati, mwenzake wa Sotik Bw Dominic Koskei na Mwakilishi
wa Kike kaunti ya Bomet, Bi Joyce Korir walisema kumekuwa na malalamishi mengi kutoka kwa wanachama kwamba hata baada ya kujiuzulu kutoka Jubilee, imekuwa vigumu kuhamia vyama vingine vya kisiasa.
Baadhi ya wale ambao wamejiuzulu wamejipata wamerejeshwa chamani na kulazimika kuacha mchakato huo tena.
“Msajili wa vyama vya kisiasa anafaa kushughulikia malalamishi kutoka kwa wapigakura na wanaotaka kujiunga na chama cha UDA ili kuhakikisha haki zao za kidemokrasia hazikiukwi,” alisema Bw Tanui.
Bi Korir na Bw Koskei walidai kwamba imekuwa vigumu kwa wale waliojiuzulu kutoka Jubilee kujiunga na UDA huku wakikosa kupata matokeo katika e-citizen kuthibitisha vyama walivyo wanachama wavyo.
“Chochote kile kinachofanya kuwa vigumu kwa mtu kujisajili na kuthibitisha chama chake cha kisiasa kinapaswa kutatuliwa
Hali hii inatishia kufungia nje wafuasi wa UDA wakati wa mchujo kwani watazingatiwa wao si wanachama
UDA kaunti ya Bomet Bw Stephen Mutai, shida ya uhamaji ilisababishwa na ukweli kuwa Afi – si ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa ilipendelea mfumo wa dijitali.
“Katika nchi hii tuna asilimia 10 ya watu katika tovuti ya e-citizen unaotumiwa kujiuzulu, kuhama au kusajili wanachama wa chama cha kisiasa,” alisema Bw Mutai, ambaye alikuwa Naibu Gavana wa Bomet.
Bw Mutai ambaye kwa mwaka mmoja uliopita amekuwa akijihusisha na kampeni ya kusajili wanachama wa UDA katika eneo la Kusini mwa Rift Valley anadai shida hiyo imekuwapo kwa miezi kadhaa iliyopita kwa kuwa awali ilikuwa rahisi kuhama.
“Wapigakura wengi maeneo ya mashambani ambao hawana akaunti za e- Citizen wanafaa kuruhusiwa kujisajili kama wanachama wa vyama vya kisiasa na maelezo yao kukubaliwa na kupakiwa kwenye sajili. Ni haki ya kila mtu kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa,” alisema Bi Korir.
Jubilee na UDA vimekuwa vikizozania wanachama, mzozo unaotarajiwa kuongezeka kabla ya mchujo wa vyama vya kisiasa.
Jubilee ilidai kwamba UDA ilidukua hifadhi yake ya data na kuiba habari ya zaidi ya wanachama 2 milioni kisha kikawasajili kama wanachama wake.
Msajili wa vyama vya kisiasa Anne Nderitu alisema kwamba afisi yake hushughulikia maom – bi 40,000 hadi 50,000 ya kujiuzulu vyamani kila siku uchaguzi mkuu unapokaribia.
haraka kwa kuwa litakuwa suala kuu wakati wa mchujo wa vyama vya kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu ujao,” alisema Bw Koskei.
Next article
Afueni wanafunzi wa msitu wa Boni wakirejea shuleni