Connect with us

General News

Serikali yawasuta wanaopinga ujenzi wa nyumba nafuu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali yawasuta wanaopinga ujenzi wa nyumba nafuu – Taifa Leo

Serikali yawasuta wanaopinga ujenzi wa nyumba nafuu

NA FARHIYA HUSSEIN

SERIKALI imewasuta wale wanaopinga ujenzi wa nyumba za bei nafuu Mombasa, na kuwataja kuwa maadui wa maendeleo.

Katibu Mkuu katika wizara ya Nyumba na Ustawi wa Miji, Bw Charles Hinga, aliwarai wakazi wa Mombasa kupuuza wale wanaopinga ujenzi katika mtaa wa Buxton na kusema mradi huo ni mojawapo ya ile ilinayonuiwa kuleta mabadiliko nchini kwa manufaa ya umma.

“Msiruhusu watu wawili au watatu kupinga jambo linalopaswa kuleta heshima ya nchi yetu. Hawawakilishi Wakenya wengi bali maslahi yao ya kibinafsi. Wengi wao wana zaidi ya nyumba mbili na wengine wanamiliki nyumba katika fuo za bahari hivyo basi wanapinga maendeleo ya wananchi,” akasema.

Alikuwa akizungumza alipokagua mradi huo wa Buxton Point unaoendelezwa na kampuni inayohusishwa na mfanyabiashara Suleiman Shahbal.

Bw Shabal aliiomba serikali kushirikiana na mabenki ili kuhakikisha Wakenya wanapata mikopo nafuu ya kununua nyumba hizo ambazo awamu ya kwanza ya ujenzi inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni.

Awamu hiyo ya kwanza itapelekea nyumba 582 kuwasilishwa kwa wamiliki waliozilipia.

“Tumejenga nyumba nzuri za bei nafuu lakini tunaomba serikali iwezeshe wananchi wake, hasa wakazi wa Mombasa kusaidiwa kwa mikopo nafuu ya kununua nyumba hizo,” akasema Bw Shahabal.

Aidha, Bw Hinga alithibitisha kuwa mipango inaendelea serikalini kushirikiana na

Shirika la Kitaifa la Makao (NHC) ili kuwapa wapangaji mikopo ya umiliki wa nyumba kwa viwango vya riba vya chini.

“Tunazingatia mchakato ambapo wanaweza kupata mikopo. Wapo wanaofanya biashara ndogo ndogo ambao hawapokei mshahara mwisho wa mwezi. Tunaangalia mchakato ambapo wanaweza kupata mikopo kwa riba ya asilimia tatu, wanunue nyumba na kulipia kwa muda wa miaka 20 au 30,” akasema katibu huyo.

Miradi sawa na hiyo ya kujenga nyumba za kisasa za bei nafuu inaendelezwa katika maeneo mengine Mombasa ikiwemo Likoni, kando na sehemu mbalimbali za nchi.

Bw Hinga alisema nyumba nyingi chini ya mpango huo zishaanza kujengwa na baadhi kukamilika, lakini ufadhili zaidi wahitajika ili kufanikisha malengo ya serikali kikamilifu.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending