Connect with us

General News

Siri ya kupunguza unene na uzani uliopitiliza – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Siri ya kupunguza unene na uzani uliopitiliza – Taifa Leo

Siri ya kupunguza unene na uzani uliopitiliza

Na MARGARET MAINA

[email protected]

IKIWA unahisi unasumbuliwa na uzani na unene uliopitiliza, basi uko katika hatari ya kusumbuliwa na shida nyingi za kiafya, pamoja na ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa ini lenye mafuta, ugonjwa wa nyongo, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, na aina fulani za saratani.

Unaweza ukajitoa kwa tatizo hili.

Kula vizuri kiafya

Chagua protini zenye nyuzi badala ya mafuta. Protini ni muhimu kwa sababu husaidia katika kujenga misuli na viungo kufanya kazi ipasavyo. Punguza ulaji wa nyama nyekundu. Ondoa ngozi kutoka kwa kuku kabla ya kuipika.

Usipende kula chakula chenye mafuta mengi kama vya kukaangwa au kuweka mafuta mengi kwenye chakula.

Kwenye mboga, unaweza kupata protini nyingi kutoka kwa soya, karanga, maharagwe, na mbegu. Dengu, kunde, na maharagwe ni vyanzo bora vya nyuzi na protini.

Tumia maziwa yenye mafuta kidogo kama chanzo cha protini, pamoja na jibini la mafuta kidogo na mtindi. Kwa upande wa vitafunio, tumia ndizi, viazi, na maboga.

Kula matunda na mboga zaidi

Matunda husaidia kukidhi ladha ya utamu katika kinywa chako kwa kuwa yana sukari yake ya asili. Matunda na mboga huwa na nyuzi zinazosaidia uhisi umeshiba haraka.

  • Kula matunda na mboga mboga katika kila mlo hata asubuhi wakati ukila vitafunwa. Kula celery, karoti, pilipili, broccoli au koliflawa kama saladi.
  • Viazi vitamu, na mchele wa kahawia huongeza nguvu mwilini.
  • Kidokezo muhimu: Kumbuka kwamba mkate mweupe, unga uliosindikwa na ule wa ugali, na hata sukari nyeupe hukupa nguvu haraka lakini kuna hatari yake kwa sababu hugeuka kuwa mafuta haraka sana.
  • Kula chakula cha wanga ya asili badala ya kilichosindikwa. Ukiweza, epuka vyakula vilivyosindikwa kama mkate mweupe, tambi au keki.

Kuwa na ratiba au mpango rasmi wa lishe

  • Zingatia lishe bora na ule samaki, dagaa, matunda na mboga, mayai, mbegu na karanga.
  • Punguza chumvi kwenye lishe yako
  • Ulaji wa chumvi kupindukia husababisha mwili wako kubaki na maji, ambayo yanaweza kusababisha ujisikie umefuriwa tumbo na kupata uzani uliopitiliza. Badala ya chumvi, jaribu kuoka chakula chako na pilipili.