Connect with us

General News

Janga la njaa ni baya zaidi Kaskazini, mashirika yalia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Janga la njaa ni baya zaidi Kaskazini, mashirika yalia – Taifa Leo

Janga la njaa ni baya zaidi Kaskazini, mashirika yalia

NA JACOB WALTER

MAAFISA wakuu katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wametoa tahadhari kuhusu ukame ambao unaendelea kukeketa maeneo ya Kaskazini mwa Kenya na maeneo mengine yanayoshuhudia ukame.

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), Beth Bechdol na Afisa Mratibu wa UNCT, Stephen Jackson walieleza hofu yao kuhusu ukame ambao umeathiri sana Kaunti ya Marsabit.

Akizungumza wakati wa kusambaza malisho ya mifugo eneo la Teso, Kaunti-ndogo ya Moyale, Bi Bechdol alisema serikali haijachukua hatua madhubuti kupambana na ukame huo ambao umesababisha kifo cha zaidi ya mifugo 150,000.

“Huu ni wakati wa kusaidia wafugaji hasa wanakijiji. Hata hivyo, matukio ambayo yanaendelea kushuhudiwa ya vifo vya mifugo na maisha ya raia kuwa hatarini yanazua janga la kibinadamu,” akasema Bi Bechdol.

Mvua imekuwa ikikosa kushuhudiwa katika maeneo mengi ya Kaskazini Mashariki mwa Kenya huku wakazi wengi wakilemewa na njaa kwa sababu ya ukosefu wa vyakula na maji.

Bi Bechdol alisema kuna haja ya kuongeza huduma za dharura kwa kuwa magatuzi ya maeneo hayo hayawezi kustahimili athari ya ukame huo kutokana na ukosefu wa fedha. Pia alitoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa jamii za wafugaji

ambazo zimeathirika zinasaidiwa hasa kupitia mpango wa ununuzi wa mifugo. Aidha, serikali pia ilishauriwa izamie miradi ambayo itasaidia kubadilisha hali ya kiuchumi na anga ndipo eneo hilo la Kaskazini Mashariki lijitegemee kiuchumi.

Kwa upande wake, Bw Jackson alisema kuwa mashirika mbalimbali ya kijamii yanafaa yaongeze ufadhili katika juhudi za kuwanusuru raia kutokana na athari za ukame.

“Iwapo tutazidisha juhudi zetu, tutawasaidia sana Wakenya wengi hasa kutoka Kaskazini Mashariki. Hili ni janga ambalo limekwepo na limekuwa likitatiza nchi kwa miaka mingi,” akasema Bw Jackson.

Zaidi ya familia 2,500 katika Kaunti ya Marsabit zinakumbwa na njaa huku zikiwa zimepoteza mifugo yao yote wala hazina njia ya kujizimbulia riziki. Zaidi ya Wakenya milioni 1.7 pia wanakumbwa na njaa.

Bi Bechdol alisisitiza kuwa jukumu la kupambana na ukame huo halifai kuachiwa mashirika ya kutoa misaada na serikali pekee bali pia hata wanasiasa wa eneo hilo.

Kadhalika, alisifu mpango wa serikali wa ununuzi wa mifugo kutoka hasa Kaunti ya Marsabit ambapo wafugaji wameathiriwa vibaya. Majuma mawili yaliyopita mbunge wa North Horr, Bw Chachu Ganya alieleza kuwa njaa hiyo imesababisha kifo cha mtu mmoja katika eneobunge lake huku mamia ya mifugo pia ikifa kwa kukosa malisho.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending