Connect with us

General News

Menengai na Strathmore kikaangoni Kenya Cup – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Menengai na Strathmore kikaangoni Kenya Cup

Menengai na Strathmore kikaangoni Kenya Cup

Na GEOFFREY ANENE

Macho yatakuwa kwa mduara wa nne-bora kwenye Ligi Kuu ya Raga (Kenya Cup) ambapo Menengai Oilers na Strathmore Leos watakuwa na mtihani mgumu, Jumamosi.

Viongozi Kabras Sugar watavaana na nambari nne Strathmore ugani Kakamega Showground nao nambari mbili na mabingwa watetezi KCB na nambari tatu Oilers watapepetana uwanjani KCB Ruaraka. Timu hizo nne tayari zinaonekana zimeshafuzu kushiriki nusu-fainali.

Zinajipanga kuhakikisha zinakamilisha msimu wa kawaida katika nafasi nzuri. Timu mbili za kwanza zitakuwa wenyeji wa nusu-fainali. Inatarajiwa pia washindi wa msimu wa kawaida wataandaa fainali wasipobanduliwa katika nusu-fainali.

Baada ya mechi nane za kwanza, Kabras wanaongoza kwa alama 40 wakifuatiwa na KCB (36), Oilers (33) na Strathmore (30). Ratiba (Februari 12): Mwamba vs Nondies (1pm, Jamhuri Park), Homeboyz vs Impala Saracens (3pm, Jamhuri Park), KCB vs Menengai Oilers (3pm, Ruaraka), Blak Blad vs Kenya Harlequin (3pm, Kenyatta University), Topfry Nakuru vs Masinde Muliro (3pm, Nakuru Athletic), Kabras Sugar vs Strathmore Leos (3pm, Kakamega Showground).