Connect with us

General News

Serikali yalemewa kukabili majangili Kerio – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali yalemewa kukabili majangili Kerio – Taifa Leo

Serikali yalemewa kukabili majangili Kerio

NA FRED KIBOR

SERIKALI inaonekana imelemewa katika kupambana na majangili katika Bonde la Kerio, eneo la Bonde la Ufa licha ya operesheni inayoendelea ya kuwatimua.

Katika siku mbili zilizopita, majangili hao walitekeleza mashambulizi mengi eneo la Marakwet na kumjeruhi mchungaji mmoja kisha kutoweka na mamia ya mifugo.

Mnamo Jumatano, majangili hao walivamia lokesheni ya Murkutwo na kuvamia wachungaji malishoni kisha kuiba mifugo ambayo idadi yake haijulikani na pia kumjeruhi

Bw Amos Kibet. Akiwa na majeraha kifuani na mapajani, Kibet anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Rufaa (MTRH), Eldoret.

Alhamisi majangili wanaodaiwa kutoka jamii ya Pokot walimvamia Flora Suter nyumbani kwake Tot

kisha na kuiba mbuzi 80. Pia waliiba pikipiki iliyopatikana baadaye katika kituo cha kibiashara cha Tot.

Uvamizi huo wa majangili umekuwa ukiendelea wakati ambapo manaibu kamishina kutoka eneo hilo wamekuwa wakiandaa mikutano na wenyeji kutoka jamii za Marakwet na Pokot kutafuta amani.

“Kuna operesheni zinazoendelea na tuna hakika kuwa tutawapata majangili waliohusika na wizi huo wa mifugo. Tumeshauriana na wazee ili kuzidisha kampeni za kuhakikisha kuwa kuna amani na kupunguza visa hivi,” akasema Mshirikishi, Bw Maalim Mohamed.