Connect with us

General News

Seneti kuhoji Yatani kuhusu kuchelewa kwa pesa za kaunti – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Seneti kuhoji Yatani kuhusu kuchelewa kwa pesa za kaunti – Taifa Leo

Seneti kuhoji Yatani kuhusu kuchelewa kwa pesa za kaunti

NA GEORGE MUNENE

WAZIRI wa Fedha Ukur Yatani anatarajiwa kufika mbele ya Seneti kutokana na kucheleweshwa kwa Sh72 bilioni za kaunti.

Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti kuhusu Fedha na Bajeti Charles Kibiru, alisema Waziri ataagizwa kufika mbele ya kamati hiyo wiki ijayo kufafanua ni kwa nini Hazina ya Kitaifa imechukua muda mrefu kutoa fedha hizo. Alieleza kuwa ucheleweshaji huo umelemaza huduma katika kaunti.

Akizungumza na wana – habari mjini Sagana, Bw Kibiru ambaye pia ni Seneta wa Kirinyaga alimshutumu Waziri kwa kuvunja sheria kwa kukosa kutoa fedha hizo kwa wakati ufaao..

Alisema kaunti zinakabiliwa na wakati mgumu kifedha na haziwezi kuendeleza shughuli ipasavyo.

“Kwa sasa, baadhi ya kaunti zimeshindwa kununulia hospitali dawa. Hospitali hizo pia hazina vifaa vingine muhimu za maabara kama vile bendeji na hata chakula cha wagonjwa.

Wagonjwa katika kaun – ti mbalimbali wanalalamika kuwa wanatumwa katika maduka ya kibinafsi kununua dawa,” alisema Bw Kibiru.

Wakenya wamekuwa wakilalamikia kuhusu barabara mbaya katika kaunti hasa baada ya msimu wa mvua.

“Tutamlazimisha Yatani kujiwasilisha mbele ya Kamati.

Waziri anatarajia kaunti ziendeleze vipi shughuli zao na kuwahudumia Wakenya vyema bila pesa,” alihoji Bw Kibiru.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending