Connect with us

General News

Wakulima zaidi wajitokeza kuuzia NCPB mahindi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakulima zaidi wajitokeza kuuzia NCPB mahindi – Taifa Leo

Wakulima zaidi wajitokeza kuuzia NCPB mahindi

NA BARNABAS BII

IDADI ya wakulima ambao wanawasilisha mahindi yao kwenye Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB), imeongezeka mara mbili katika muda wa wiki mbili zilizopita.

Hii ni baada ya NCPB kudumisha bei ya Sh3,000 kwa kila gunia la kilo 90 licha ya kushuka kwa bei ya mahindi sokoni.

NCPB imenunua magunia 50,000 ya kilo 90 kutoka kwa idadi ya awali ya magunia 20,000 huku wakulima ambao wamekuwa wakiyahifadhi mahindi yao, nao wakijitokeza na sasa kuyauza.

Kujitokeza huko kwa wakulima kumechangiwa na bei kupungua kwa Sh400 kuto – ka Sh3,200 hadi Sh2,800, hii ikichangiwa na kuongezeka kwa mahindi yanayoingizwa nchini kutoka Uganda na Tanzania.

“Tumeamua kudumisha bei yetu ya kununua kila gunia kwa Sh3,000 licha ya kupungua kwa bei sokoni,” akasema Meneja Mkurugenzi wa NCPB, Bw Joseph Kimote.

Bodi hiyo imekuwa ikipokea magunia 3,000 ya mahindi kila siku na imekuwa ikiwashawishi wakulima kwa kuwalipa hela zao haraka pamoja na pia kuwapa nafasi ya kuhifadhi mahindi yao katika bohari ya bodi hiyo.

Kwa mujibu wa Bw Kipng’etich Mutai ambaye ni mwenyekiti wa Muungano wa kampuni za kusaga mahindi wa Grain Belt, wamiliki wa kampuni za kusaga mahindi wameamua kupunguza gharama zao kutokana na idadi ndogo ya Wakenya wanaonunua unga wa kupikia ugali.

“Baadhi ya watumiaji bidhaa wameamua kujisagia unga wa mahindi,” akasema Bw Mutai.