[ad_1]
Seneta Kibiru ajitosa kuwania ugavana
NA GEORGE MUNENE
SENETA wa Kirinyaga Charles Kibiru, ametangaza azma yake ya kuwania ugavana katika Kaunti hiyo kupitia tiketi ya chama cha Jubilee.
Bw Kibiru alitangaza hilo Jumamosi alipozindua rasmi kampeni yake, akilenga kumbandua Gavana Anne Waiguru, ambaye yupo katika kambi ya Naibu Rais Dkt William Ruto na atatetea wadhifa wake kupitia UDA.
Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Kirinyaga Wangui Ngirici pia analenga kiti cha ugavana japo kama mwaniaji huru na imekuwa ikifasiriwa kuwa ushindani mkali utakuwa kati yake na Bi Waiguru.
Hata hivyo, Bw Kibiru alisema aliamua kuwania kiti hicho baada ya kujisaili kwa undani, huku
akiahidi kuwahudumia vyema wakazi wa Kirinyaga. Alipuuza madai kuwa ni Bi Ngirici na Gavana Waiguru ambao wapo katika nafasi nzuri ya kutwaa kiti hicho.
“Mnamo 2017, niliwania kama mwaniaji huru na kushinda kiti cha Useneta. Mara hii nitawania kwa tiketi ya Jubilee na naamini kutokana na uungwaji mkono wa wakazi, nitapita na kuwa gavana wenu,” akasema Bw Kibiru “Watu wangu wamekuwa wakiteseka ndio maana niliamua kuwania kiti hiki ili niwasaidie,” akaongeza.
Uzinduzi huo wa kampeni ambao ulifanyika katika Shule ya Msingi ya Kang’aru eneobunge la Mwea, ulihudhuriwa na Seneta James Orengo, mwenyekiti wa ODM John Mbadi na Gavana wa Laikipia Nderitu Mureithi.
Next article
Wakulima zaidi wajitokeza kuuzia NCPB mahindi
[ad_2]
Source link