Vitunguu, nyanya na viungo vingine. PICHA | MARGARET MAINA
Paka hapo mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu kwa kiasi tu.
Katakata vitunguu maji na pilipili mboga uweke pembeni.
Kwangua kwenye mbuzi nyanya na karoti halafu nazo uweke pembeni.
Katakata majani ya giligilani vipande vidogo uweke pembeni.
Andaa kikaangio na jiko.
Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi. Yakishachemka, weka vitunguu maji na kaanga hadi vilainike na viiva (hakikisha haviungui).
Weka pilipili mboga na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika.
Sasa weka vipande vya nyama, koroga na funikia kwa dakika tatu kisha weka nyanya zako na weka chumvi kisha koroga ili zichanganyike vizuri. Ni zamu yako kuweka majani ya giligilani na pilipili kama utapenda.
Acha vichemke kwa dakika tano. Hakikisha moto sio mkali sana.
Weka viungo vyako na ufunike.
Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako.
Pakua kwenye bakuli na katakata majani ya giligilani uweke kwa juu.
Unaweza kula kwa ugali, wali, au chochte ukipendacho.