Connect with us

General News

Yadaiwa Gicheru alitoa hongo ya mamilioni kwa mashahidi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Yadaiwa Gicheru alitoa hongo ya mamilioni kwa mashahidi – Taifa Leo

ICC: Yadaiwa Gicheru alitoa hongo ya mamilioni kwa mashahidi

NA VALENTINE OBARA

UPANDE wa Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), jana ulieleza kuwa unataka kuthibitisha jinsi baadhi ya mashahidi waliibuka kuwa mamilionea ghafla, walipojiondoa kwa kesi iliyomwandama Naibu Rais William Ruto.

Hilo liliibuka huku Wakili Paul Gicheru anayekabiliwa na mashtaka manane kuhusu madai ya kushawishi mashahidi kujiondoa katika kesi hiyo ya ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007, akifikish – wa mahakamani jana, ambapo alikanusha mashtaka yote dhidi yake.

Kulingana na upande wa mashtaka, upelelezi uliofanywa katika akaunti za benki za baadhi ya mashahidi ulibainisha kuwa, kiasi cha pesa kiliongezeka ghafla kwa viwango vya kutisha.

Imedaiwa kuwa, mmoja wa mashahidi aliyekiri kuandamwa na kikundi cha Bw Gicheru ili ajiondoe kwa kesi ya Dkt Ruto, alikuwa na Sh297 pekee katika akaunti yake lakini kiwango hicho kikaongezeka kwa muda mfupi mno.

Akisoma taarifa za baadhi ya mashahidi, wakili wa upande wa mashtaka, Bw Anton Steynberg, alisema watathibitisha kwamba pesa hizo zilikuwa ni hongo kutoka kwa Bw Gicheru ambaye amedaiwa alikuwa anamwakilisha Dkt Ruto katika njama hizo.

“Rekodi za benki zitathibitisha aliweka pesa nyingi kwa akaunti siku ile ile ambayo alituambia alipokea pesa hizo. Kwanza alilipwa hongo ya Sh500,000 akasema alitumia Sh100,000 na kuhifadhi Sh400,000. Baada ya siku chache akaweka Sh400,000 na hivyo kwa jumla alihongwa kwa Sh900,000,” akaeleza Bw Steynberg.

Imedaiwa mashahidi walihongwa viwango tofauti vya pesa, hadi Sh5 milioni.

Taarifa ya shahidi mwingine ilieleza kuwa, kikundi hicho cha Bw Gicheru kilimwandama na kumwambia walipokea ripoti alikuwa shahidi na walitaka ajiondoe.

Upande wa mashtaka umedai kuwa, mashahidi wengine walitishiwa ili wajiondoe na mienendo hiyo ndiyo ilifanya kesi dhidi ya Dkt Ruto na mwanahabari Joshua Sang iwe dhaifu hadi ikasitishwa.

Kesi hiyo iko mbele ya Jaji Miatta Maria Samba wa mahakama ya ICC iliyo The Hague, Uholanzi.

Wapelelezi wa ICC walikuwa wakiendeleza uchunguzi kuhusu kuhongwa kwa mashahidi, wakati ambapo kesi ya Dkt Ruto ilikuwa bado inaendelea.

Katika upelelezi huo, mashahidi walioripoti kwa ICC kwamba waliandamwa ili wajiondoe, waliombwa na wapelelezi kuwa wajifanye watakubali pendekezo hilo huku wakiwa wanarekodi mazungumzo yao na watu waliodaiwa kumwakilisha naibu rais.

Shahidi wa kwanza aliyeitwa mahakamani jana amedaiwa kuwa miongoni mwa waliokataa kuhongwa na badala yake wakasaidia kwa ukusanyaji wa ushahidi.