Connect with us

General News

Jubilee yamkataa mshukiwa wa ufisadi wa NYS – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jubilee yamkataa mshukiwa wa ufisadi wa NYS – Taifa Leo

Jubilee yamkataa mshukiwa wa ufisadi wa NYS

NA ERIC MATARA

CHAMA cha Jubilee jana kilikataa ombi la mshukiwa katika kesi ya kashfa ya Idara ya Huduma ya Kitaifa ya Vijana (NYS), Anne Wambere Ngirita ya kujiunga na chama hicho ili kuwania kiti cha Mwakilishi wa Kike Kaunti ya Nakuru.

Chama hicho kilimtaka Bi Ngirita apate kibali kutoka kwa taasisi za serikali kwanza kabla ya kuomba tiketi ya chama hicho.

Bi Ngirita aligonga vichwa vya habari mnamo 2015 alipohusishwa kwenye wizi wa mamilioni ya pesa za NYS. Kesi ya ufisadi dhidi yake inaendelea.