Connect with us

General News

Ruto na wandani wake wasisahau awali walitetea serikali kwa kukopa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ruto na wandani wake wasisahau awali walitetea serikali kwa kukopa – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Ruto na wandani wake wasisahau awali walitetea serikali kwa kukopa

MUUNGANO wa Kenya Kwanza (KKA) unaoongozwa na Naibu Rais William Ruto umeisuta serikali ya sasa kwa kukopa kupita kiasi na hivyo kuongeza mzigo wa madeni ambao sasa umefikia Sh8.2 trilioni.

Wamedai kiwango cha madeni kilianza kupanda kwa kiwango kikubwa mno baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuridhiana kisiasa na kiongozi wa ODM Raila Odinga, katika kile kilichotajwa kama ‘handisheki’.

Lakini Dkt Ruto, mbunge wa Garissa Mjini Aden Duale, na wenzao, wasije wakasahau kati ya miaka ya Juni 2013 na Februari 2018 walikuwa watetezi sugu wa mwenendo wa serikali kukopa kwingi.

Kwa mfano, Dkt Ruto akiongea katika kituo cha kibiashara cha Kiawara, Kaunti ya Nyeri alisema hivi: “Tunakopa kwa nidhamu, mipango na tuna miradi ambayo tungetaka kutekeleza kwa manufaa ya wananchi.”

Awali, kati ya 2014 na 2016 Naibu Rais alitetea vikali mkopo wa Eurobond wa kima cha Sh278 bilioni.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending