Connect with us

General News

Ruto apata pigo wandani wake wakiamua kujiunga na Jubilee – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ruto apata pigo wandani wake wakiamua kujiunga na Jubilee – Taifa Leo

Ruto apata pigo wandani wake wakiamua kujiunga na Jubilee

NA STEPHEN ODUOR

NAIBU Rais William Ruto, amepata pigo baada ya wandani wake katika Kaunti ya Tana River kumhepa.

Mbunge wa Bura, Bw Ali Wario na Seneta Juma Wario, walitangaza hawataki tena kushirikiana na Chama cha United Democratic Alliance (UDA), kwa vile wameamua kujiunga na Chama cha Jubilee.

Wawili hao walikuwa mstari wa mbele kupanga kampeni za UDA katika kaunti hiyo.Bw Wario ambaye amepanga kuwania ugavana Tana River, jana alisema alifanya uamuzi huo, baada ya kukutana na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi wiki iliyopita.