Connect with us

General News

Utaratibu usio na maumivu makali wa kuondoa uvimbe wa ‘fibroids’ – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Utaratibu usio na maumivu makali wa kuondoa uvimbe wa ‘fibroids’ – Taifa Leo

Utaratibu usio na maumivu makali wa kuondoa uvimbe wa ‘fibroids’

NA PAULINE ONGAJI

Uterine fibroid embolization (UFE), ni utaratibu wa kimatibabu dhidi ya uvimbe wa fibroid. Utaratibu huu hausababishi maumivu na unahusisha mwongozo wa picha na tayari wagonjwa wengi humu nchini wamefanyiwa.

Manufaa makuu ya utaratibu huu kwa wanawake ni kwamba mkato ni wa ukubwa wa milimeta 2 na kwamba wanaweza rejea kazini katika kipindi cha wiki moja baada ya utaratibu huu.Fibroid, ni uvimbe ambao japo hausababishi kansa, sio wa kawaida.

Uvimbe huu huota kwenye uterasi ya mwanamke katika miaka yake ya uzazi. Kulingana na utafiti, asilimia 80 ya wanawake hukumbwa na uvimbe huu wanapotimu miaka 50.Kuna aina tofauti za uvimbe huu na hutambulika kulingana na eneo la uterasi lililoathirika.

Ili kutambua aina ya uvimbe, mwaathiriwa anapaswa kuchunguzwa na mwanajinakolojia ili afanyiwe uchunguzi wa fupanyonga (pelvis). Uchunguzi huu hutumika kutambua hali, saizi na umbo la uterasi yake.

Kwa hivyo, tiba hutolewa kuambatana na umri wa mgonjwa, saizi ya uvimbe na kwa ujumla hali ya afya ya mhusika.

UFE hutekelezwa na mwanarediolojia ambaye huingiza mrija mdogo kwenye mkato mdogo wa ukubwa wa milimeta 2 juu ya mguu au kwenye kifundo cha mkono, na kuusukuma kwa utaratibu kupitia ateri ya uterasi, kisha kuingiza chembechembe ndogo(Polyvinyl Alcohol Particles-PVA) kwenye ateri zinazosambaza damu kwa uterasi na uvimbe.

Chembechembe hizi huzuia usambazaji wa damu kwenye uvimbe, na hivyo kusababisha kunywea na kufa.

Utaratibu huu ni salama kwa wanawake wanaotaka kushika mimba baadaye, japo unashauriwa kusubiri kwa kati ya miezi sita na mwaka mmoja, kabla ya kushika mimba.