Connect with us

General News

Buffon sasa kuchezea Parma hadi afike umri wa miaka 46 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Buffon sasa kuchezea Parma hadi afike umri wa miaka 46 – Taifa Leo

Buffon sasa kuchezea Parma hadi afike umri wa miaka 46

Na MASHIRIKA

KIPA wa zamani wa Italia, Gianluigi Buffon, amerefusha mkataba wake katika klabu ya Parma hadi 2024, kumaanisha kwamba atakuwa ametimu umri wa miaka 46 kufikia wakati ambapo kandarasi hiyo itatamatika.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia kwa sasa ana umri wa miaka 44 na alisajiliwa na Parma inayoshiriki Ligi ya Daraja ya Pili nchini Italia (Serie B) kwa mkataba wa miaka miwili mwishoni mwa msimu wa 2020-21.

Buffon alishinda mataji 10 ya Serie A akivalia jezi za Juventus na anajivunia rekodi ya kucheza mechi 657 katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Buffon alianza kusakata soka kitaaluma akichezea Parma mnamo Novemba 1995 na amedakia kikosi hicho mechi 23 za Serie B kufikia sasa muhula huu. Waajiri wake hao wanakamata nafasi ya 13 katika orodha ya vikosi 20 baada ya kupiga jumla ya michuano 26.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending