Connect with us

General News

Ni undumakuwili kwa wabunge wa UDA kutumia pesa za umma safarini Amerika – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ni undumakuwili kwa wabunge wa UDA kutumia pesa za umma safarini Amerika – Taifa Leo

CHARLES WASONGA: Ni undumakuwili kwa wabunge wa UDA kutumia pesa za umma safarini Amerika

NA CHARLES WASONGA

KARANI wa Bunge la Kitaifa Michael Sialai amefichua kuwa bunge limegharimia nauli za wabunge sita walioandamana na Dkt Ruto katika ziara yake nchini Amerika, safari ambayo ni sehemu ya kampeni zake za urais.

Wengine walioandamana naye ni; Kimani Ichung’wa Aden Duale (Garissa Mjini), Alice Wahome (Kandara), Owen Baya (Kilifi Kaskazini), Beatrice Adagala (Mwakilishi wa Kike, Vihiga) na Soipan Tuya (Narok).

Kwa mujibu wa sheria kuhusu usimamizi wa fedha, bunge hugharimia safari za wabunge wanapoenda ng’ambo kwa shughuli zinazohusiana na majukumu yao kama wabunge.

Baada ya kurejea kutoka ziara kama hizo, wao huhitajika kuandaa ripoti ambazo huwasilishwa bungeni na kujadiliwa.

Swali langu ni je, ni ripoti gani ambayo Bw Ichung’wa na wenzake wataandaa pindi watakaporejea kutoka ziara hiyo ya siku 10 katika nchi za Amerika na Uingereza?Asasi ya bunge na Wakenya walipaushuru watafaidi vipi kutokana na ziara hii?

Ama kwa hakika Afisi ya Naibu Rais ilivunja sheria kwa kuomba bunge lifadhili safari za wabunge hawa sita. Kwa upande wake, bunge la kitaifa lilikosea kwa kukubali ombi hilo kwa sababu azma ya safari hiyo haioani na majukumu ya wabunge hao.

Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Nancy Gathungu sasa ana kibarua cha kuchunguza suala hili kwani pesa ambazo hutengewa Tume ya Huduma za Bunge (PSC) hazifai kutumika kugharimia kampeni za urais za afisa wa serikali ambaye si mbunge au mfanyakazi wa asasi hiyo.

Kinaya ni kwamba juzi tu wabunge hawa wa Kenya Kwanza wakiongozwa na Bw Ichung’wa walipendekeza kubuniwe kwa Hazina Maalum ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo walioathiriwa na Covid-19.

Ni kielelezo kuwa endapo Dkt Ruto atashinda katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, serikali yake itatekeleza sera za kuinua maisha ya masikini walio wengi.

Lakini kwa kutumia pesa za umma kugharimia ziara zao za kampeni ng’ambo, Dkt Ruto na wandani wake wameonyesha wazi kuwa ubadhirifu wa pesa utakita katika serikali yao.