Connect with us

General News

Raila kuchapa kampeni kali Ruto akiwa ng’ambo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Raila kuchapa kampeni kali Ruto akiwa ng’ambo – Taifa Leo

Raila kuchapa kampeni kali Ruto akiwa ng’ambo

JUSTUS OCHIENG NA BENSON MATHEKA

KIONGOZI wa chama cha ODM Raila Odinga amepanga kampeni kali ya siku 10 kuanzia kesho itakayokamilika kwa mkutano mkubwa jijini Nairobi Jumamosi Machi 12 ambapo inatarajiwa atatangazwa rasmi mgombea urais wa muungano wa Azimio la Umoja.

Bw Odinga atafanya kampeni hiyo wakati Naibu Rais William Ruto yuko nje ya nchi kwa kipindi cha siku kumi.

Baada ya chama cha Jubilee kuidhinisha muungano wake na ODM, mnamo Jumamosi wiki jana, Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kuwa ataanza kampeni kali ya kumpigia debe Bw Odinga kama mgombea urais wa muungano wa Azimio la Umoja.

Bodi ya kampeni ya Bw Odinga inayoongozwa na Gavana wa Laikipia Ndiritu Muriithi, jana ilitoa ratiba inayoonyesha kwamba waziri mkuu huyo wa zamani ataanza kampeni katika kaunti ya Nakuru Jumatano ambapo anatarajiwa kuungana na Rais Kenyatta kwa kampeni mara ya kwanza baada ya vyama vyao kuidhinisha ushirikiano wao.

Naibu Rais William Ruto na washirika wake katika muungano wa Kenya Kwanza unaojumuisha Musalia Mudavadi (Amani National Congress) na Moses Wetang’ula (Ford Kenya) pia walizindua kampeni yao ya pamoja katika kaunti ya Nakuru mnamo Januari 26, siku tatu baada ya kutangaza ushirikiano wao katika mkutano wa kitaifa wa wajumbe wa ANC uliofanyika katika jumba la Bomas of Kenya Januari 23.

Jana, Bw Denis Onsarigo, ambaye ni Katibu wa afisi ya kampeni ya Bw Odinga, alisema kwamba kuna mazungumzo yanayoendelea ili Rais Kenyatta ahudhurie baadhi ya mikutano ya Bw Odinga.

“Siwezi kuzungumza kwa niaba ya Jubilee lakini kuna mazungumzo yanayoendelea kuhusu hayo. Iwapo uamuzi utafanywa, tutafurahia rais akiandamana nasi,” Bw Onsarigo aliambia Taifa Leo jana.

“Tutakuwa na kampeni kali ya kisiasa kwa muda wa wiki mbili,” alisema. Baada ya Nakuru Bw Odinga atazuru kaunti za Kisii na Nyamira kabla ya kuelekea kaunti ya Machakos Ijumaa Machi 4 na Bungoma mnamo Jumamosi Machi 5.

“Jumapili, Machi 6 Bw Odinga ataelekea kaunti ya Nyeri kwa kampeni na Machi 8 tutakuwa Maralal, kaunti ya Samburu,” alifi – chua Bw Onsarigo.

Kaskazini Mnamo Machi 9, kampeni za vuguvugu la Azimio zitaelekea kaunti ya Wajir kabla ya kutua Busia Alhamisi Machi 10.

“Mnamo Machi 12, kutakuwa na Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wa Azimio jijini Nairobi,” alieleza Bw Onsarigo.

Ni katika mkutano huo mkubwa ambapo Bw Odinga atatangazwa mgombea urais wa Muungano wa Azimio la Umoja.

Bw Odinga anaonekana kutumia siku kumi ambazo mshindani wake mkuu kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 Naibu Rais William Ruto atakuwa katika ziara ng’ambo.

Dkt Ruto na baadhi ya washirika wake katika muungano wa Kenya Kwanza wanaojumuisha Bw Mudavadi, jana walianza ziara Amerika kabla ya kuelekea Uingereza. Katika nchi hizo mbili, Dkt Ruto atakutana na maafisa wa serikali na Wakenya wanaoishi huko.