Connect with us

General News

Narc Kenya yaomba muda zaidi kabla ya kutia saini makubaliano ya OKA – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Narc Kenya yaomba muda zaidi kabla ya kutia saini makubaliano ya OKA – Taifa Leo

Narc Kenya yaomba muda zaidi kabla ya kutia saini makubaliano ya OKA

Na CHARLES WASONGA

CHAMA cha Narc Kenya kinachoongozwa na Martha Karua sasa kimeomba siku saba zaidi ili kiweze kuchambua nakala ya makubaliano ya kuundwa rasmi kwa Muungano wa One Kenya Alliance (OKA) kabla ya kuamua ikiwa kitaitia saini au la.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Jumanne, Machi 1, 2022, Katibu Mkuu wa chama hicho Orwa Michael, alisema Baraza la Kuu la Kitaifa (NEC) ya chama hicho litatumia muda huo kuchambua masharti kwenye kielelezo cha makubaliano hayo.

“Baada ya kupokea nakala ya makubaliano kuhusu suala hilo saa 36 zilizopita NEC imekubaliana kwamba inahitaji muda zaidi kuchunguza stakabadhi hiyo na nyinginezo kuhusu suala hili,” akasema Bw Orwa.

“Jopo la wataalamu katika chama cha Narc Kenya limeagizwa kusaka ufafanuzi kuhusu masuala fulani ambayo hayaeleweki katika stakabadhi hiyo kabla ya kuandaa ripoti itakayowasilishwa kwa NEC baada ya siku sababu ili iweze kuidhinishwa,” akasema Bw Orwa kwenye taarifa hiyo aliyoitoa baada ya kamati ya NEC kukutana mjini Naivasha.

Vyama vingine tanzu katika muungano wa OKA ni; Wiper, Kanu, na United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo.

Hata hivyo, Bw Orwa alieleza kuwa sababu iliyochangia Narc Kenya kuomba kuahirishwa kwa shughuli ya kutiwa saini kwa mkataba wa makubaliano wa kurasimisha OKA ni pamoja na sheria mpya ya Vyama vya Kisiasa.

“Sheria hii inafaa kutafsiriwa na kuchunguzwa kwa makini,” Katibu huyo Mkuu akasema.

Kwa mujibu wa mipango ya awali, vyama tanzu katika OKA vilipangiwa kutia saini makubaliano ya kurasimisha muungano huo mnamo Jumatano, Machi 2, 2022.