Connect with us

General News

Raia 1,000 wa Ukraine wakwama Zanzibar – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Raia 1,000 wa Ukraine wakwama Zanzibar – Taifa Leo

Raia 1,000 wa Ukraine wakwama Zanzibar

NA MASHIRIKA

ZANZIBAR, TANZANIA

WATALII zaidi ya 1,000 raia wa Ukraine, wamekwama hotelini Kisiwani Zanzibar huku mapigano yakichacha katika nchi yao.

Waziri wa Utalii wa Zanzibar Leila Mohammed Mussa, jana alisema kuwa raia hao wa Ukraine wamekwama katika hoteli mbalimbali kisiwani hapo.

Kulingana na Waziri Mussa, wengi wa watalii hao wanataka kurejea nyumbani kutangamana na familia zao licha ya nchi yao kuendelea kumiminiwa mabomu na majeshi ya Urusi.

Alisema kuwa serikali ya Tanzania tayari imewasiliana na balozi wa Ukraine nchini Kenya ambaye amekubali kuwasafirisha watalii hao ku – toka Zanzibar hadi mataifa jirani na Ukraine kama vile Poland.

“Kwa sasa watalii hao wanapewa huduma hotelini na kuliwazwa kuwa wako mahali salama hawafai kuwa na wasiwasi,” Bi Mussa akaambia wanahabari.

Jana, wizara ya Usalama ya Ukraine ilisema kuwa raia wa nchi hiyo 80,000 waliokuwa wanaishi ughaibuni wamerejea nyumbani kupigana na majeshi ya Urusi.

Taarifa ya wizara ilisema kuwa wengi waliorejea ni wanaume na tayari wamepewa silaha na kwenda kuungana na wanajeshi wa nchi hiyo katika uwanja wa vita.

Naibu waziri wa Usalama wa Ukraine Pawel Szefernaker, alisema kuwa raia 450,000 wa nchi hiyo, wametorokea nchini tangu Urusi kuvamia taifa hilo la Ulaya siku sita zilizopita.

Jana, Urusi iliendeleza mashambulio katika majengo ya miji mbalimbali nchini Ukraine.

Wanajeshi wa Urusi walitangaza kuteka nyara mji wa Kherson ulio na jumla ya watu 300,000 kusini mwa Ukraine.

Shirika la habari la UNIAN, jana liliripoti kuwa roketi za kivita za Urusi, zilishambulia jengo la polisi mjini Kharkiv. Picha zilizochapishwa mtandaoni na mshauri wa serikali ya Ukraine, Anton Geraschenko, zilionyesha jengo hilo la polisi likiteketea.

Geraschenko alisema jengo hilo linamilikiwa na Chuo Kikuu cha Karazin. Serikali ya Ukraine pia ilithibitisha kuwa watu wawili waliuawa na wengine wengi wakajeruhiwa mjini Zhytomyr baada ya kuangukiwa na kombora kutoka kwa wanajeshi wa Urusi.

Gavana wa mji wa Kharkiv, Oleg Synegubov, jana alisema kuwa watu 21 waliuawa katika eneo hilo baada ya majeshi ya Urusi kuangusha bomu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, hata hivyo, alidai kuwa majeshi yake yamefanikiwa kuua wanajeshi 6,000 wa Urusi.

Umoja wa Mataifa (UN) unasema kuwa raia 140 wa Ukraine wameuawa katika mapigano hayo. Lakini Ukraine inasisitiza kuwa idadi ya raia waliouawa ni zaidi ya 300.

Tayari makali ya mapigano nchini Ukraine yameanza kuhisiwa kote duniani kufuatia kuongezeka kwa bei ya mafuta na mbolea.

Vikwazo ambavyo Urusi im – ewekewa na jamii ya kimataifa pia vimeanza kuathiri raia wa nchi hiyo. Serikali ya Urusi tayari imepiga marufuku raia wake kusafiri nje ya nchi huku wakiwa wamebeba zaidi ya Sh1 milioni.