Connect with us

General News

Bodaboda wagomea ada ya maegesho – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Bodaboda wagomea ada ya maegesho – Taifa Leo

Bodaboda wagomea ada ya maegesho

NA DAVID MUCHUI

SERIKALI ya Kaunti ya Meru hupoteza mamilioni ya fedha kama mapato kufuatia hatua ya maelfu ya wahudumu wa bodaboda waliokataa kulipa ada hitajika.

Kulingana na ripoti kuhusu hali ya maeneo ya maegesho ndani ya mji wa Meru iliyotayarishwa na Kamati ya Bunge la kaunti hiyo kuhusu Fedha, wahudumu wa bodaboda huwa hawalipi ada za maegesho. Hii ni licha ya kwamba kulingana na sheria wanapaswa kulipa ada ya Sh20 kila siku au Sh300 kila mwezi.

Meneja wa Manisipaa ya Meru Mbaabu Muguna aliambia Taifa Leo kwamba kuna karibu wahudumu wa bodaboda 4,000 ambao huhudumu katika zaidi ya maegesho 20 mjini Meru pekee.

Hii ina maana kuwa serikali ya kaunti ya Meru hupoteza karibu Sh80,000 kila siku, mapato ambayo ingekusanya kutoka kwa wahudumu wa bodaboda ambao huhudumu mjini Meru pekee.

Kulingana na takwimu za sensa ya 2019, asilimia 9.8 ya familia katika Kaunti ya Meru humiliki pikipiki za uchukuzi. Hii ina maana kuwa kuna zaidi ya pikipiki 40,000.

Inakisiwa kuwa kuna jumla ya wahudumu 30,000 wa boda boda katika kaunti yote ya Meru. Endapo watalipa Sh20 kila siku kama ada ya maegesho, Sh600,000 zitakusanywa kila siku.