Connect with us

General News

Karan Patel ndiye mfalme wa Nakuru Rally – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Karan Patel ndiye mfalme wa Nakuru Rally – Taifa Leo

Karan Patel ndiye mfalme wa Nakuru Rally

Na GEOFFREY ANENE

DEREVA Karan Patel anaendelea kufanya vyema kwenye Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) baada ya kuzoa taji la Nakuru Rally, Jumamosi.

Akielekezwa na Tauseef Khan, Patel alitawala kilomita 155.34 za kushindania pointi baada ya kurejesha gari lake la Ford Fiesta R5 wa kwanza kwa saa 2:01:27.0.

Patel hakuwa ameshinda mbio zozote katika mashindano 40 ya kwanza tangu ajitose katika fani hii mwaka 2014, sasa ameshinda duru tatu kati ya saba zilizopita na mbili mfululizo baada ya kuonyesha wenzake kivumbi Kajiado Rally mwezi Januari.

Jasmeet Chana akishirikiana na Ravinder Chana katika gari la Mitsubishi Evo10 amemaliza Nakuru Rally katika nafasi ya pili kwa saa 2:07:16.4 naye Hussein Malik/Deep Patel wakafunga mduara wa tatu-bora kwa saa 2:13:23.8. Ghalib Hajee/Ismail Riyaz (Mitsubishi Evo10), Kush Patel/Mudasar Chaudry (Subaru Impreza Wagon), Zameer Verje/Zahir Shah (Subaru Impreza) na Leonardo Varese/Kigondu Kareithi (Toyota Auris) walifuatana kutoka nafasi ya nne hadi saba mtawalia.

Madereva Aakif Virani, Issa Amwari, Stephen Mwangi na Daren Miranda wote walijiuzulu. Duru ya Nakuru ilivutia madereva 14, ingawa 11 ndio walianza mashindano.