Connect with us

General News

Ongeri akashifu waliomzoma katika mkutano wa Azimio – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ongeri akashifu waliomzoma katika mkutano wa Azimio – Taifa Leo

Ongeri akashifu waliomzoma katika mkutano wa Azimio

Na RUTH MBULA

SENETA wa Kisii Sam Ongeri amekashifu tukio ambapo viongozi kutoka eneo hilo walizomewa wakati wa mkutano wa muungano wa Azimio la Umoja ulioongozwa na kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Profesa Ongeri ambaye ni miongoni mwa viongozi waliozomwa na umati wakati wa mkutano huo, alisema siasa za makabiliano huenda zikaathiri maadili ya jamii ya Abagusii.

Wakati wa mkutano huo, seneta huyo, waziri wa zamani Chris Obure, Mwakilishi wa Kike Janet Ongera na aliyekuwa mbunge wa Mugirango Kusini walizomewa na hotuba zao zikakatizwa.

Hayo yote yalifanyika mbele ya Bw Odinga na viongozi wengine kutoka maeneo mbalimbali nchini waliohudhuria mkutano huo.

“Siasa za makabiliano zinazochipuza katika jamii yetu zinaiharibia sifa yetu. Tunafaa kuwa watu watulivu na wanaovumilia misimamo tofauti,” akasema.

Wakati wa msururu wa mikutano ya Azimio la Umoja iliyofanyika katika kaunti za Kisii na Nyamira, Bw Odinga alishuhudia viongozi kadhaa wakidhulumiwa na umati. Raia hao walionekana kutofurahishwa na viongozi wao kutokana na sababu ambazo hazikubainika waziwazi.

“Kwa hivyo, nawaomba muwe na nidhamu. Na ikiwa hamtaonyesha heshima, mtagharimia mienendo hiyo,” Profesa Ongeri akafoka baada ya umati kumzomea.

Seneta huyo aliongeza: “Nitawaambia, tumekuja hapa kuunga mkono Raila Odinga. Mwaweza kupiga kelele nyingi mnavyoweza lakini hamtaenda popote. Hii ni kwa sababu tutakutana debeni na tutaona yule ambaye ataibuka mshindi.”

“Kile tunachoshuhudia ni kundi la watu ambao wamelipwa ili wapige kelele. Lakini nawaambia kuwa hamtakuwa na maisha mazuri siku za usoni,” Profesa Ongeri alionya.

Sawa na Profesa Ongeri, Bw Obure alikaripiwa vikali na wananchi mbele ya Bw Odinga. Alinyimwa nafasi ya kuwahutubia maelfu ya wafuasi waliojitokeza kukutana na Bw Odinga.

Profesa Ongeri na Bw Obure wanapania kumrithi Gavana wa Kisii James Ongwae ambaye anahudumu muhula wake wa pili na wa mwisho.

Lakini wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu katika kampeni zao kutokana na upinzani mkali wa Mbunge wa Dagorreti Kaskazini Simba Arati.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending