[ad_1]
Ulawiti: Mwalimu aachiliwa korti ikikosa ushahidi
NA BRIAN OCHARO
MWALIMU aliyeshtakiwa kwa madai ya kulawiti wanafunzi wake wakati wa masomo ya ziada, ameachiliwa huru.
Hakimu Mkazi wa mahakama ya Mombasa, Bw Martin Rabera, aliamua kuwa hakuna ushahidi kuthibitisha kuwa, Bw Elphas Mukangali alifanya makosa hayo.
Upande wa mashtaka ulikuwa umedai kuwa, mshtakiwa alilawiti wanafunzi wawili ambao alikuwa akiwafanyia masomo ya ziada mnamo Aprili 26, 2019.
[ad_2]
Source link