Connect with us

General News

Kisa cha Forest Road kisitumiwe kuwachukulia wanabodaboda wote kama wahalifu – Raila – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kisa cha Forest Road kisitumiwe kuwachukulia wanabodaboda wote kama wahalifu – Raila – Taifa Leo

Kisa cha Forest Road kisitumiwe kuwachukulia wanabodaboda wote kama wahalifu – Raila

NA CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa ODM Raila Odinga ameonya dhidi ya kile anachosema ni kulaumiwa kwa wahudumu wote wa bodaboda nchini kufuatia kisa ambapo mwendesha gari mmoja wa kike alidhulumiwa katika barabara ya Wangari Maathai (zamani Forest Road), Nairobi.

Akihutubia mkutano wa vuguvugu la Azimio la Umoja katika uwanja wa michezo wa Maua, kaunti ya Nairobi Bw Odinga alisema wahudumu wengine wa bodaboda kote nchini wasiwekewe makosa yaliyotendwa na wachache miongoni mwao.

“Isichukuliwe kuwa bodaboda wote nchini walihusika katika kisa hicho cha kinyama. Mtu akitenda kosa, mtu huyo anafaa kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria,” Bw Odinga alisema.

Waziri huyo Mkuu wa zamani alisisitiza kuwa sio vizuri kwa sekta yota ya bodaboda kuathirika na makosa ya sehemu ndogo ya wahudumu hao.

“Mtu akifanya kosa, isichukuliwe kuwa kila mhudumu wa bodaboda ni mhalifu. Kuna wengi wao ambao ni waadilifu na huzingatia sheria katika biashara hii,” Bw Odinga akasema.

Hata hivyo, alilaani kitendo hicho ambapo kundi la wahudumu wa bodaboda walimshambuliwa mwanamke huyo ambaye ni mhudumu wa ubalozi wa Zimbabwe.

Hii ni kufuatia kisa ambapo gari la raia huyo wa kigeni liligongana na pikipiki ya mhudumu mmoja wa bodaboda Ijumaa wiki jana saa kumi na moja jioni.

“Naalaani kabisa kitendo hicho na wahusika wote wanafaa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Hawa ndio wachache ambao wanawaharibia sifa wahudumu hawa ambao hutegemea biashara hii kujikimu,” Bw Odinga akasema.

Mhudumu wa bodaboda kwa jina Zachary Nyaoga Obadia ndiye ametambuliwa na maafisa wa polisi kama kiongozi wa kundi la wanabodaboda waliomshambulia mwanamke huyo na kumdhulumu kimapenzi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending