Connect with us

General News

Ukatili wa bodaboda ulichora picha halisi ya Mkenya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ukatili wa bodaboda ulichora picha halisi ya Mkenya – Taifa Leo

WANDERI KAMAU: Ukatili wa bodaboda ulichora picha halisi ya Mkenya

NA WANDERI KAMAU

MARA nyingi, vitendo vya wanadamu husawiri uhalisia wa jamii wanakoishi.

Vitendo hivyo pia husawiri historia na utamaduni wa kimienendo wa jamii hiyo.

Hivyo, wakati jamii inaweka msingi mbaya wa kimaadili, inapaswa kujilaumu yenyewe wakati kizazi ama vizazi vyake vinapopotoka.

Narejelea ghadhabu zilizoibuka nchini dhidi ya wahudumu wa bodaboda, kutokana na kisa ambapo baadhi yao walinaswa wakimdhulumu dereva mwanamke katika Barabara ya Prof Wangari Mathai, jijini Nairobi.

Kwenye kisa hicho ambacho kimeibua hisia kali nchini, wahudumu hao walimshambulia mwanamke huyo na kumraruria nguo zake kiasi cha kuonyesha uchi wake.

Cha kushangaza ni kuwa, wahudumu hao walionekana kutojali hata kidogo, licha ya mwanamke huyo kupiga kamsa akiomba usaidizi.

Kulingana na utaratibu wa uumbaji wake Mungu, mwanamume ameumbwa akiwa mwenye nguvu ili kumlinda na kumtetea mwanamke. Mwanamke ni kama kama chombo cha kuendeleza uumbaji.

Yeye ndiye huhimili uchungu wa kumbeba mtoto kwa miezi tisa na baadaye kumzaa katika mazingira magumu. Ni vipi tunaweza kuwakosea hekima viumbe muhimu kama hao? Maovu makuu yanayoiandama Kenya kwa sasa ni wizi, tamaa na ufisadi.

Wizi na ufisadi ni kama saratani anayougua kila Mkenya, mkubwa kwa mdogo.

Ingawa raia wa kawaida wamekuwa wakitoa malalamishi kuhusu “tamaa” miongoni mwa watu wenye ushawishi kama vile wanasiasa, wao wenyewe ndio wanafaa kujilaumu. Lazima tuweke misingi itakayokemea maovu na kutilia mkazo thamani na umuhimu wa maadili.

[email protected]