Connect with us

General News

Waandalizi wa Ballon d’Or wabadilisha kanuni, vigezo vya kutafutwa kwa mshindi wa tuzo hiyo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Waandalizi wa Ballon d’Or wabadilisha kanuni, vigezo vya kutafutwa kwa mshindi wa tuzo hiyo – Taifa Leo

Waandalizi wa Ballon d’Or wabadilisha kanuni, vigezo vya kutafutwa kwa mshindi wa tuzo hiyo

Na MASHIRIKA

MSHINDI wa taji la Ballon d’Or ambalo hutolewa kwa mwanasoka bora zaidi wa kiume na wa kike duniani sasa ataamuliwa kutokana na matokeo yake katika msimu mmoja badala ya kalenda ya mwaka mzima jinsi ambavyo imekuwa.

France Football ambao ni waandalizi wa tuzo hiyo ya haiba kubwa wameamua pia kupunguza idadi ya waamuzi au majaji wanaohusika kutafuta mshindi.

Jopo la wanahabari 170 ambao wamekuwa wakihusika awali sasa litakuwa na wanahabari 100 pekee watakaotafuta mshindi wa wanasoka wa kiume huku waamuzi 50 pekee wakihusika katika kusaka mshindi wa kike. Wanahabari hao wanatokea katika mataifa yanayoshikilia nafasi za juu kwenye orodha ya viwango bora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

“Hapo awali, kigezo tulichotumia ni matokeo ya wanasoka katika nusu mbili za kampeni za msimu mmoja. Washindi wapya sasa watapatikana kutegemea matokeo yao kila msimu,” akasema mhariri wa jarida la France Football, Pascal Ferre kwa kusisitiza kwamba mabadiliko hayo yanachochewa na haja ya kuondoa utata na kurahisisha zaidi mchakato wa kutafuta mshindi wa kila kitengo au kategoria.

Hatua ya Lionel Messi wa Paris Saint-Germain (PSG) na timu ya taifa ya Argentina kutawazwa mshindi wa Ballon d’Or mnamo 2021 ilizua mjadala mkali huku mashabiki, wachanganuzi na wadau wengi wa soka wakihisi kwamba Robert Lewandowski wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland ndiye alistahili kutwaa taji hilo.

Messi aliweka rekodi ya kutwaa taji hilo kwa mara ya saba licha ya Lewandowski aliyeambulia nafasi ya pili kufunga mabao 41 katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) na kusaidia Bayern kuzoa taji la Bundesliga kwa mara ya tisa mfululizo.

Kwa mujibu wa Ferre, kitakachozingatiwa zaidi ni matokeo ya mwanasoka binafsi uwanjani badala ya idadi ya mataji yatakayokuwa yamenyanyuliwa na klabu au timu ya mchezaji.

Tuzo ijayo ya Ballon d’Or itatolewa mnamo Septemba au Oktoba 2022 na itategemezwa kwenye matokeo ya msimu utakaokamilika mnamo Julai kwa kipute cha Euro 2022 miongoni mwa wanawake. Ina maana kwamba fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Qatar kati ya Novemba na Disemba hazitachangia kupatikana kwa mshindi taji hilo kwa upande wa wanasoka wa kiume.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending