Connect with us

General News

Wito serikali iondoe ada za juu katika viwanja bora wanamichezo wapate fursa ya kufanya mazoezi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wito serikali iondoe ada za juu katika viwanja bora wanamichezo wapate fursa ya kufanya mazoezi – Taifa Leo

Wito serikali iondoe ada za juu katika viwanja bora wanamichezo wapate fursa ya kufanya mazoezi

NA SAMMY WAWERU

BINGWA wa mbio za mita 100 nchini, Ferdinand Omanyala ameiomba serikali kuondoa ada zinazotozwa katika nyanja za michezo kufanya mazoezi ili kusaidia kukuza vipaji.

Staa huyo amesema ada za juu zinazotozwa ili wanamichezo waruhusiwe kutumia majukwaa ya michezo Kenya, zinazima ndoto za baadhi wasio na uwezo kifedha lakini wangependa kupalilia talanta zao.

“Ukizuru viwanja vya serikali vyenye vifaa bora vya kufanyia mazoezi, ni lazima ulipie. Kikwazo cha uwanja kinazima ndoto za vijana wengi waliojaaliwa vipaji mbalimbali katika michezo,” Omanyala akasema akizungumza jijini Nairobi.

Alitoa kauli hiyo siku chache baada ya kung’aa katika awamu ya tatu ya mashindano ya Athletics Kenya uwanjani Nyayo, Nairobi.

Akikumbuka baadhi ya changamoto alizopitia wakati akipalilia kipaji chake katika mbio za kasi za mita 100, Bw Omanyala alisema ukosefu wa uwanja bora kufanya mazoezi ulimhangaisha.

“Vipaji wanaotozwa malipo, wanajipalilia talanta zao. Hawana pesa. Ingewezekana, naomba serikali iondoe ada hizo,” akahimiza.

Alitaja uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa MISC Kasarani na ule wa Nyayo, kuwa ni baadhi tu ambazo zinapaswa kutoa huduma za mazoezi bila malipo.

Aidha, gwiji huyo katika riadha alisema kuna vijana wengi mitaani waliojaaliwa talanta mbalimbali katika michezo na sanaa, japo ukosefu wa miundomsingi bora inazima na kuzuia kuafikia ndoto zao.