Connect with us

General News

Afueni kaunti ikizindua kituo cha upasuaji – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Afueni kaunti ikizindua kituo cha upasuaji – Taifa Leo

Afueni kaunti ikizindua kituo cha upasuaji

NA STEPHEN ODUOR

WAKAZI wa eneobunge la Bura, Kaunti ya Tana River, wanatarajia kupata afueni baada ya serikali ya kaunti kuzindua kituo cha kwanza maalumu cha upasuaji wa uzazi.

Gavana wa Tana River, Bw Dhadho Godhana amewahakikishia wakazi kwamba kituo hicho kipya cha Bura kitakuwa kikiwatolea huduma bora za matibabu.

Kwa muda mrefu, wakazi wa eneo hilo walikuwa wakilazimika kutafuta huduma za upasuaji kwa kaunti jirani ya Garissa.

Kulingana nao, wamekuwa wakipoteza baadhi ya jamaa zao wajawazito kila wanapokabiliwa na matatizo wakati wa kujifungua.

“Tudumishe umakini wetu katika kuendeleza hospitali zetu, kuifanya sekta ya afya kuwa kipaumbele kuanzia hospitali kuu hadi zahanati ya mashinani,” akasema gavana.