Connect with us

General News

Si haki kuzidi kupuuza elimu ya mtoto maskini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Si haki kuzidi kupuuza elimu ya mtoto maskini – Taifa Leo

TAHARIRI: Si haki kuzidi kupuuza elimu ya mtoto maskini

NA MHARIRI

KWA miaka michache sasa, serikali ya kitaifa imekuwa ikiangazia sana hitaji la kutekeleza kikamilifu mfumo mpya wa elimu ya CBC.

Chini ya mipango hiyo, mojawapo ya masuala makuu ambayo yamepewa kipaumbele ni ujenzi wa madarasa mapya yatakayofanikisha masomo bila kutatiza wanafunzi, mbali na kutoa mafunzo ya ziada kwa walimu kuhusu mbinu mpya za kufundisha watoto.

Licha ya kuwa hatua zimepigwa katika juhudi hizo zote, bado kuna tatizo la tangu jadi ambalo ni lazima wadau wa elimu walishughulikie kwa dharura.

Tatizo hilo ni kuhusu pengo kubwa lililopo kati ya mandhari ya kimasomo kwa watoto wanaotoka familia zinazojiweza kifedha, na wale wanaotoka katika familia maskini.

Inafahamika kuwa, mojawapo ya malengo ya kuanzisha CBC ilikuwa ni kuondoa ushindani ambao umekuwepo kila mara mitihani ya kitaifa inapofanywa.

Hata hivyo, pengo la ubora wa kielimu kati ya jamii tofauti bado litaendelea kuwepo hata kama mitihani hiyo itaondolewa ikiwa hakuna mikakati itakayoekwa kujaribu kuleta usawa kwa kiasi cha haja.

Ni aibu sana tunaposhuhudia kuwa katika karne hii, bado kuna watoto ambao wanatatizika sana kupokea elimu bora kwa sababu ambazo zinaweza kutatuliwa.

Changamoto kama vile uhaba wa madarasa au ukosefu wake, miundomsingi duni, ukosefu wa vifaa vya kuelimisha watoto na uhaba wa walimu ni mambo ambayo yanahitajika kupewa kipaumbele na serikali yoyote ile inayojali maslahi ya wananchi wake.

Ripoti huonyesha jinsi rasilimali nyingi za fedha hutengwea masuala ya elimu kuanzia kutoka kwa serikali ya kitaifa, za kaunti, hadi chini ya Hazina ya Serikali ya Kitaifa ya Kustawisha Maeneobunge (NG-CDF) iliyo chini ya wabunge.

Inashangaza fedha hizo zote zinazosemekana kutengewa elimu kila mwaka huwa zinafanyiwa nini hasa katika maeneo ya nchi ambapo mateso ya watoto kupata elimu bora yamekuwa kama ibada.

Wakati huu ambapo serikali kupitia kwa Wizara ya Elimu iko mbioni kujenga madarasa mapya ya CBC, wadau wasisahau kuna matatizo yale ya tangu jadi ambayo yanahitaji kusuluhishwa.

Bila hilo, tutakuwa tunaendelea kuwekeza kwa mfumo wa elimu ambao utazidi kubagua watoto maskini katika jamii.

Elimu hasa ya msingi ni mojawapo ya haki zinazolindwa sana katika sheria za nchi na za kimataifa kwa hivyo ni muhimu masuala haya yachukuliwe kwa uzito unaostahili.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending